Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk.
Jabiri Bakari,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao
umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi
Serikalini.
Baadhi ya waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa usikivu Taarifa ya Mtendaji
Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma wakati akitoa
taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi
ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wakala
wa Serikali Mtandao wakifuatilia taarifa ambayo ilikuwa inatolewa na
Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog
………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAKALA wa Serikali Mtandao
umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za
Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini
ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji
Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,wakati akiongea na waandishi wa
habari leo jijini Dodoma amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa
matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.
Dk.Bakari amesema kuwa wameamua
kutumia utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni
dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza
ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma.
Aidha amesema kuwa kuwa mfumo
huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za
utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa
idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.
Dk.Bakari amesisitiza kuwa
mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi
nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi,
ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti.
“Pia utawezesha usimamizi wa
majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji
wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za
utendaji”amesema Dk.Bakari
Hata hivyo amesema kuwa mfumo
huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata
taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.
Dk. Bakari amesema kuwa mfumo
huo wa ERMS unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo
mingine mikuu ya serikali ikiwemo Mfumo Mkuu wa Uhasibu, Mfumo wa
Usimamizi wa Taarifa za Rasilimaliwatu (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya
Serikali Kieletroniki (GePG), Mfumo wa Barua pepe Serikalini (GMS) na
Mfumo wa Ofisi Mtandao.
Pia amesisitiza kuwa moduli za
mfumo huo zinaweza kuongezwa au kupunguzwa bila kuathiri utendaji kazi
wa moduli nyingine au mfumo kwa ujumla.
Amezitaja baadhi ya mifumo
mingine ambayo wakala umeitengeneza katika utekelezaji wa jitihada za
serikali mtandao ambao ni tovuti kuu ya serikali, tovuti kuu ya ajira,
mfumo wa barua pepe serikalini ambao unatumiwa na taasisi za umma 402
zikiwemo ofisi za ubalozi nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana taarifa
serikalini.
Aidha Dk. Bakari amezitaka
taasisi za umma kuendelea kutumia tehama katika kuboresha utendaji kazi
serikani na utoaji huduma kwa umma kwa kuzingatia miongozo na viwango
vya serikani mtandao
No comments:
Post a Comment