Pages

Tuesday, April 2, 2019

UJENZI WA KITUO CHA AFYA MNAZI MMOJA WALETA FURAHA WILAYANI LINDI


1 1A index
Baadhi ya Majengo mapya ya Kituo cha Afya Mnazi Mmoja
2
Waziri Jafo akiwa na baadhi ya viongozi na wananchi katika kituo cha Afya Mnazi mmoja
………………………..
Wananchi wa eneo la Mnazi Mmoja Katika Wilaya ya Lindi wameishukuru Sana Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajengea kituo cha afya cha Kisasa Sana katika eneo lao. Shukran hizo zilitolewa leo April 2 wakati wa Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI wilayani humo alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayo simamiwa na TAMISEMI.
ujenzi wa Kituo cha Afya Mnazi mmoja kimeleta ukombozi kwa wananchi wa eneo hilo kwani
kwa muda mrefu wamekuwa wakitaabika sana kufuata huduma bora za afya katika hospitali ya Mkoa Lindi ambayo ipo mbali kutokea eneo hilo.
Katika ziara hiyo waziri Jafo amewapongeza viongozi na wananchi wa wilaya ya Lindi kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Hata hivyo Jafo amewasisitiza wananchi kutunza miundombinu iliyojengwa.

No comments:

Post a Comment