Bi. Neema Mtemvu, Afisa
Uhusiano (TBS), akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibaoni
wakati TBS ilipotembela shuleni hapo kutoa elimu juu bidhaa hafifu.
Wanafunzi wa shule ya
sekondari Kwashungu, wakisikiliza elimu juu ya masuala yahusuyo viwango
vya ubora, kutoka kwa maafisa Wa TBS.
Bi.Amina Yasin, Afisa
Udhibiti ubora Mwandamizi (TBS), akizungumza na wajasiriamali wilayani
kilombero kuhusiana na utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.
Bi Amina Yasin, Afisa
Udhibiti Ubora Mwandamizi(TBS) akizungumza na wananchi wa soko kuu la
Ifakara, wilayani Kilombero, juu ya umuhimu wa kununua bidhaa
zilizothibitishwa ubora wake na TBS.
……………………………..
Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) limetembelea shule ya sekondari Kibaoni pamoja na Shule
ya sekondari ya Kwashungu wakati wa Kampeni yake ya kuelimisha umma juu
ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizo na ubora katika Wilaya ya
Kilombero.
Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS) akizungumza na wanafunzi pamoja na
walimu, amefafanua umuhimu wa viwango katika
maisha yao ya kila siku vilevile kuwafahamisha fursa ya huduma bure kwa
wajasiriamali wadogo.Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS) akizungumza na wanafunzi pamoja na
Bi Gradness amesisitiza
kuwa jukumu la kupiga vita bidhaa hafifu katika Taifa ni la kila mtu,
hivyo aliwaasa wawe mabalozi wazuri wa kuhamasisha ubora katika jamii
wanazoishi.
Kwa upande wake, Mwalimu
mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaoni, Bw. Kalinga aliwapongeza TBS kwa
kufika shuleni hapo kwani ni mkakati mzuri ukizingatia shule huwa na
wanafunzi wengi na wanaoishi maeneo mbalimbali hivyo ikiwa kila mmoja
atasambaza ujumbe huo kwa ndugu jamaa na marafiki utakuwa umewafikia
watu wengi kwa muda mfupi. Mwalimu Kalinga pia hakuacha kutoa wito kwa
TBS kuendelea na zoezi hilo kwani linajenga msingi mzuri kwa vizazi
vijavyo na kutengeneza jamii yenye tamaduni ya kujali ubora.
Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma pia ilifanyika katika Soko kuu la Ifakara lenye viunga 515 na maduka 105, pamoja na maeneo ya madukani Ifakara mjini, huku jumla ya wanafunzi 2,089 na walimu 78 wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Ubora .
Sambamba na hayo, TBS ilitoa semina kwa wajasiriamali wapatao 23 katika ukumbi wa halmashauri ya mji Ifakara, ambapo Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza wajasiriamali kufuata utaratibu waliolekezwa ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure bila gharama yoyote, kwani ni fursa ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji kuweza kushindana na kuuza ndani na nje ya nchi . Vilevile wasisite kutuma maombi TBS kwa ajili ya kupata mafunzo maalum yatolewayo kwa wajasiriamali.

No comments:
Post a Comment