Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika eneo la Kiwanda na
Shamba la Miwa Mbigiri linalohudumiwa na Gereza la Mbigiri wakati wa
ziara ya kutembelea mradi huo mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akisikiliza maelezo yanayohusu
maendeleo ya Shamba la Miwa Mbigiri linalohudumiwa na Gereza la Mbigiri
wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo mkoani Morogoro.Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
……………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Serikali imetoa onyo kwa
wafanyabiashara au mtu yoyote mwenye nia ya kuhujumu Miradi ya
Serikali kwa maslahi binafsi kuacha mara moja na endapo mtu
atathibitika kuhusika na
suala hilo sheria kali zitachukuliwa dhidi
yao.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo alipotembelea
Kiwanda na Shamba la Miwa katika Gereza la Mbigiri ambalo
linakadiriwa kuzalisha tani za sukari Laki Mbili kwa Mwaka na kuondoa
adha ya kuagiza sukari nje ya nchi.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kukuza viwanda mbalimbali ikiwemo kiwanda cha Sukari
Mbigiri na kuwezesha mamia ya wananchi kupata ajira pamoja na kukuza
uchumi wa nchi.
“Kuna taarifa za baadhi ya
wafanyabiashara wakubwa wa sukari kupenyeza maslahi yao binafsi katika
miradi hii mikubwa ya serikali ikiwemo shamba hili la miwa hapa Mbigiri,
nawaasa waache mara moja kwani watakapobainika hatua kali za kisheria
zitachukuliwa juu yao ikiwemo na kosa la uhujumu uchumi” alisema Masauni
Akitoa taarifa ya shamba hilo
Mkuu wa Gereza Mbigiri, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Shija Fungwe
alisema shughuli zinaendelea katika shamba hilo kwa kutumia nguvu kazi
ya wafungwa kutoka katika gereza hilo huku wafungwa 280 wakitumika
katika shamba hilo.
“Kazi ya kupanda eneo lililo
tayari inaendelea huku kazi ya kulima hekta 500 inaendelea na kati ya
hizo hekta 200 zimeshalimwa kwa awali na lengo letu ikifika mwezi juni
mwaka huu inatakiwa zilimwe hekta 700 tukitumia nguvu kazi ya wafungwa”
Alisema ACP Fungwe
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameelekeza
kubadilishwa kwa Mjumbe wa Bodi ya Kiwanda hicho, ACP Rocky Mbena
anaewakilisha Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment