Pages

Monday, April 1, 2019

PROF NDALICHAKO AZINDUA JENGO JIPYA LA KUFUNDISHIA CHUO CHA KUMBUKUMBU MWALIMU NYERERE


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako akizungumza kabla ya kufungua Jengo la kufundishia la Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako(Katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo Jipya la Kufundishia lililojengwa na chuo hicho kwa gharama za mapato ya Ndani
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako Akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephene Wasira wakifungua Kitambaa katika jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la kufundishia.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephene Wasira akizungumza na wadau wa elimu na Wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa Jengo Jipya la kufundishia lililojengwa na chuo hicho katika Kampasi ya kivukoni

Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof. Shadrack Mwakalila akizungumza jambo juu ya hatua zilifanikisha kujenga jengo hilo
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako,akiwa ameketi ndani ya Ukumbi huo mara baada ya kufungua jengo hilo
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako akiwa ameketi katika picha ya pamoja na Viongozi pamoja Viongozi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Jengo Jipya la kufundishia la Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere linavyoonekana kwa nje


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
 
Waziri wa
Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza  Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa
kuwa mfano kwa kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kutumia vizuri mapato ya ndani katika kutekeleza miradi ya
maendeleo.
 
Mheshimiwa
Ndalichako ameyasema hayo wakati akizindua rasmi ukumbi mpya wa kisasa wa
mihadhara katika Kampasi ya Kivukoni ambapo amesema Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere kimeonyesha njia hivyo amezitaka taasisi nyingine za elimu
kuiga mfano wa Chuo hiki kwa kuthamini mapato yake ya ndani na kuelekeza fedha
hizo kwenye miradi ya maendeleo.
 
Mhe.Prof.
Ndalichako amekiagiza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kujielekeza  zaidi katika kutoa mafunzo ya uongozi  na kuongeza kuwa  kwa kushirikiana na Serikali wizara yake
itahakikisha kunakuwa na mfumo maalum wa kuhakikisha viongozi wanakuja kupata
mafunzo katika Chuo hiki.  
Akisoma
taarifa ya Chuo kuhusu mradi huo, Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila  amesema Chuo kimeamua kujenga ukumbi wa
kisasa wa mihadhara kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani.
Prof.
Mwakalila ameongeza kuwa ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 330 kwa
wakati mmoja pamoja na ofisi 8 za wafanyakazi hadi kukamilika kwake umegharimu
kiasi cha Tsh. 1,150,666,161.78.  
Aidha, Mkuu
wa Chuo ameongeza kuwa Chuo kinakabiliwa na changamoto kubwa ya ufinyu wa
bajeti ya maendeleo ambayo ingeweza kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali
ya Chuo.
 
Awali
akimkaribisha Waziri wa Elimu, Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira amesema mbali na jitihada
zinazochukuliwa na Chuo kuboresha miundombinu mbalimbali, bado Chuo kina
kabiliwa na changamoto ya miundombinu ya kutosha kukabiliana na ongezeko la
wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka.
Amesema njia
mojawapo ya kuboresha elimu ni kuwa na miundombinu rafiki bila kujali ngazi ya
elimu.
 
Mhe. Wasira
amemuomba Waziri wa Elimu kukipa kipaumbele Chuo kwa kusaidia ujenzi wa
miundombinu mbalimbali kwani mbali na Chuo hiki kubeba jina la Mwalimu Nyerere pia
ni Chuo kilichoanzishwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe.

No comments:

Post a Comment