Pages

Sunday, April 28, 2019

MAADILI NDIO MSINGI WA UTEKELEZAJI KAZINI

??
Mkuu wa Wilaya wa Mvomero Mhe. Mohamed Utaly (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Kaimu Makamu Mkuu  wa Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro(MUM) Dkt.Abdallah Yahya Tego wakielekea katika ukumbi wa Hema Jeupe kulikofanyika mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’an leo mkoani Morogoro.
??
Mkuu wa Wilaya wa Mvomero Mhe. Mohamed Utaly (wa pili kulia) akifatilia mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’an yaliyo fanyika leo katika Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro(MUM).
……………………..
Na.Majid Abdulkarim, Morogoro
Taasisi za elimu nchini zimetakiwa kuwalea wanafunzi katika maadili mema ili kuwajengea
misingi bora katika utendaji na kuleta uadilifu katika kuhudumia jamii inayowazunguka.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya wa Mvomero Mhe. Mohamed Utaly aliyemuwakilisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika leo Chuo Kikuu Cha Waislam Morogoro (MUM).
Aidha Mhe.Utaly amesisitiza kuwa taasisi za elimu kubadili mitazamo ya wanafunzi wao ili kujenga mitazamo chanya yenye kusaidia katika utendaji na kufikia malengo yanayotakiwa.
Hata hivyo Mhe.Utaly amesema kuwa ili kupata utendaji bora lazima kuwa muadilifu,mcha Mungu, kuwa na huruma kwa wale unao waongoza na kuwa mzalendo katika kuleta maendeleo endelevu .
Wakati huo huo Mhe.Utaly ameongeza kuwa kila mtanzania anawajibu wa kuimarisha maadili katika jamii inayomzunguka ili kupata watendaji waadilifu makazini na wazalendo katika kulitumikia taifa.
“Kila msomi hapa nchini anawajibu wa kuelimisha jamii inayomzunguka ili kubadili mitazamo potofu iliyo jengeka katika nyoyo za baadhi ya watu na kukemea matendo maovu ya ubakaji, ulawiti na mauaji ” Aliongezea Mhe.Utaly
Lakini pia Mhe.Utaly amesema kuwa watanzania wawe tayari kutoa ushirikiano katika kuzuia matendo maovu katika jamii ili kudumisha Amani kwa watanzania.
Mhe. Utaly ameendelea kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero inafursa mbali mbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hizo.
“Karibuni Mvomero kuna fursa ya kilimo , viwanja na nyingine nyingi ambazo zitahamasisha kuleta maendeleo katika nchi yetu” Amehitimisha Mhe.Utaly
Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu  wa chuo MUM Dkt.Abdallah Yahya Tego amesema kuwa chuo kinamalengo ya kujenga hospitali ya Rufaa Mkoani Lindi, kuanzisha kozi za uchimbaji wa gesi na mafuta na kuanzisha chuo cha Biashara Mkoani Dar es salaam.
Mashindano hayo yalianzishwa mnamo mwaka 2011na jumuiya ya kusomesha na kuhifadhi Qur’an MUM baada ya kuwa wamepata mwaliko kutoka nchini Uganda walipokwenda kushiriki katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur’an katika Chuo Kikuu cha Kiislam Uganda.

No comments:

Post a Comment