WAZIRI WA Katiba na Sheria Dkt.
Augustine Mahiga akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria
Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na wakiimba
wimbo wa mshikamano wakati wa kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
kilichofanyika jijini Arusha,
Wajumbe wa kikao cha baraza la
Wafanyakazi Wizara ya Katiba na Sheria wakiimba wimbo wa mshikamano
wakati wa kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika
jijini Arusha,
Wajumbe wa kikao cha baraza la
Wafanyakazi Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Katiba na
Sheria hayupo pichani alipokuwa akizungumza nao katika kikao cha
Baraza la Wafanyakazi Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha,
Wajumbe wa kikao cha baraza la
Wafanyakazi Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na kikao cha Baraza
la Wafanyakazi Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha,
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi
Bw. Blastus Kahemela aliesimama akizungumza wakati wa kikao cha Baraza
la Wafanyakazi Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha,
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.
Mahiga jijini Arusha wakati wa kikao cha Baraza hilo lililofanyika
Aprili 3, 2019
……………
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewaambia watumishi wa Wizara kuwa
tija na
ufanisi vitapatikana iwapo kutakuwa na maelewano na mahusiano mazuri
kati ya uongozi wa Wizara na watumishi.
Mhe. Dkt. Mahiga alipokuwa
akizungumza na Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Katiba na Sheria
lililokutana jijini Arusha kujadili masuala mbalimbali ya wizara hiyo.
Aidha Dkt Mahiga amewapongeza
watumishi hao na viongozi wao kwa kukamilisha ujenzi wa jingo jipya la
Wizara lililoko katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
“Nichukue nafasi hii kuwapongeza
kwa kazi nzuri mlioifanya ya kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya Wizara
kwa haraka na ufanisi mkubwa, hiki ni kitu cha kujivunia na binafsi
nawapongeza sana,” alisema Dkt. Mahiga.
Baraza la Wafanyakazi la Wizara
limekutana katika kikao chake cha kawaida ambacho kilipitia hija
mbalimbali ambazo uongozi wa Wizara ulizitolea maelezo juu ya namna
utekelezaji wake ulivyofanyika na hivyo kuleta tija na ufanisi katika
utendaji kazi wa wizara.
Baraza hili limefanyika chini ya
Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni
Mchome, Katibu wake Bw. Blastus Kahemela na kuhudhuriwa na Naibu Katibu
Mkuu Bw. Amon Mpanju, wajumbe wa menejimenti ya Wizara na watumishi wa
Wizara ambao ni wawakilishi wa watumishi wengine wa Wizara.
No comments:
Post a Comment