Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo (hawapo pichani)
wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu
wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (kulia)
baada ya kukamilisha muda wake wa kubadilishana uzoefu na wauguzi wa
taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Bi. Mollie amefanya kazi katika
chumba cha ICU katika taasisi ya JKCI kwa miezi 8
Mkuu
wa Kitengo cha ubora wa huduma za afya ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shemu akimpongeza Afisa Uuguzi Mwandamizi
mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa
wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie
Mullaney (kulia) kwa kushirikishana uzoefu na wauguzi wa JKCI wakati wa
hafla fupi ya kumuaga. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI
Prof. Mohamed Janabi na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
Uuguzi ya JKCI Robert Mallya
Baadhi
ya wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo
pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye
utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa
wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie
Mullaney (hayupo pichani) baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa
taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi 8 na kuagwa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert
Mallya akimkabidhi zawadi ya fremu ya kuweka picha Afisa Uuguzi
Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba
cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani
Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini
Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa
kipindi cha miezi 8. Kulia ni afisa uuguzi mwandamizi wa taasisi hiyo
Mary Haule
Afisa
Uuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule
akimwekea zawadi ya gauni juu ya mwili wake Afisa Uuguzi Mwandamizi
mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa
wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie
Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha
miezi 8.
Afisa
Uuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule
akimfunga zawadi ya kikoi Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa
kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa
hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya
kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8.
Afisa
Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika
chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini
Marekani Mollie Mullaney katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari
na wauguzi wa JKCI baada ya hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam. Bi Mollie Mullaney amefanya kazi katika chumba cha
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum katika taasisi ya JKCI kwa
kipindi cha miezi 8 na kubadilishana ujuzi na uzoefu na wauguzi wa ICI
wa taasisi hiyo.
Picha na Genofeva Matemu – JKCI
No comments:
Post a Comment