Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za
Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagala akitoa neon la ukaribisho kwa
wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na
Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za
Atomiki la kimataifaIAEA)
Naibu waziri wa Elimu,Sayansi
na Teknolojia Mh William Ole Nasha (Kulia) akifurahia jambo na
Mkurugenzi wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani Profesa Shaukat
Abdulrazak kwenye mkutano wa kimataifa unahusisha nchi 49 za kanda ya
AFRIKA.
Naibu waziri Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mh William Ole Nasha wakati akifungua mkutano wa kimataifa
unaohusisha waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya Nyuklia
kutoka nchi za kanda ya AFRIKA
Picha ikimuonyesha Naibu Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha akiwanna washiriki
wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia
ya nyuklia kutoka katika nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za
Atomiki duniani
………………………………………………………………….
Serikali ya Tanzania kupitia
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha
usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini. Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa
William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu
wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama
wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA ) unaofanyika jijini
Arusha.
Naibu waziri Ole Nasha amesema
Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbali mbali hapa
nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa vifaa
mbali mbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo
vimefungwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando jijini
Mwanza na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
Pamoja na vifaa vya uchunguzi
katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata
vifaa vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya
kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa
wataalamu katika eneo la matumizi ya mionzi na Teknolojia ya Nyuklia
mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.
Mh Ole Nasha amelishukuru na
kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya
mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano
inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama. Amewataka
washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija
kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti na matumizi salama ya
teknolojia ya nyukulia. “ majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha
mionzi na teknoljia ya Nyuklia katika Afrika inatumika vizuri kwa
maendeleo”.Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA ) Profesa Shaukat Abdulrazak
amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika
kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya Nyukilia kwenye sekta mbali
mbali ikiwemo sekta ya Afya , Kilimo,Mifugo,Maji ,Viwanda na Ujenzi.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume
ya Nguzu za Atomiki Tanzania , Profesa Lazaro Busagara amesema taasisis
yake imeendelea udhibiti na kuwachukulia hatua za kuwafungia taasisi
zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya Mionzi na Teknolojia ya
Nyuklia hapa nchini ikiwemo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi
wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia na Mionzi.
Akitoa mfano wa Hospitali amesema
mwaka 2018 walifungia hospitali 112 zilizoshindwa kufuata masharti
hayo, katika hizi tayari hospitali 40 zimekidhi na kufunguliwa huku
hospitali 72 zikiwa bado zimefungiwa kutumia vifaa vinavyotumia mionzi .
Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi 2019.
Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi 2019.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)
11/ 3/2019
Arusha, Tanzania
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)
11/ 3/2019
Arusha, Tanzania
No comments:
Post a Comment