Maandalizi ya Shughuli ya Mazishi ya Ruge Mutahaba yanaendelea Nyumbani Kwao Kabale, Bukoba ambapo ndipo Mwili utakapostiriwa.
Ujenzi wa Kabuli unaendelea kwa
kasi ambapo Fundi anathibitisha kufikia jioni Leo litakuwa limekamilika
ukiwa unasubiriwa mwili ambao utawasili jijini Dar es salaam leo kwa
ndege ukitokea Afrika Kusini ambako ndiko alikokuwa akipokea matibabu.
Baada ya kuwasili jijini Dar es
salaam Saa tisa arasili leo mwili wa marehemu Ruge utapitishwa katika
barabara za Nyerere, Mandela, Buguruni, Karume, Magomeni, Moroco Hotel,
Sinza Kijiwezi, Bamaga, ITV, Clouds ambapo utaingizwa kwa muda mfupi
katika ofisi za Clouds na kufanya sala kidogo na kisha kuondoka kupitia
barabara ya Kawe na baadaye barabara ya Mwenge kisha Utapelekwa katika
Hospitali ya Jeshi a Wananchi Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa
Kesho Mwili wa Marehemu Ruge
Mutahaba utapelekwa katika viwanja vya Karimjee na kuagwa na viongozi
mbalimbali, Wasanii Ndugu, Jamaa Marafiki na waombolezaji mbalimbali na
kisha kusafirishwa kwa ndege kurelekea mkoani Kagera siku ya jumapili
ambapo utazikwa siku ya Jumatatuo Nyumbani Kwao Kabale, Bukoba.
Vikao vya kamati vinaendelea kila
Mara kuhakikisha shughuli inakwenda kama ilivyopangwa ingawa Kuna
uwezekano wa Shughuli ya kuaga na salaam za mwisho ikafanyika uwanjani
sehemu nyingine kutokana na ufinyu wa eneo la Nyumbani eneo la mazishi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kaburi.
Baadhi ya kamaburi ya wanafamilia waliozikwa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment