JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF.
IBRAHIM HAMIS JUMA AKISALIMIANA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA
MTWARA MARA BAADA YA KUWASILI KUANZA ZIARA KATIKA MKOA WA MTWARA KWA
AJILI YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAHAKAMA
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF.
IBRAHIM HAMIS JUMA AKISAINI KITABU CHA WAGENI OFISINI KWA MKUU WA MKOA
WA MTWARA MHE. GELASIUS BYAKANWA ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE IKIWA NI
SEHEMU YA ZIARA YAKE
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKIMKABIDHI MKUU WA MKOA WA MTWARA VITABUI VINAVYOHUSU MAADILI
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF.
IBRAHIM HAMIS JUMA AKIMKABIDHI MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA MHE.
SEBASTIAN WARYUBA KITABU KINACHOELEZEA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA
MAHAKAMA YA TANZANIA PAMPOJA NA KITABU CHA MAADLI.
Lydia Churi Ntambi
…………………………..
Lydia Churi-Mahakama, Mtwara
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma ameagiza kupelekewa mashauri yote ya Mirathi nchi
nzima ili aweze kujua ni changamoto gani inayofanya yachelewe kumalizika
na
kupanga mkakati wa kisheria ili mashauri hayo yawe yanaisha ndani ya
muda uliowekwa kisheria.
Akizungumza katika ziara yake ya
kikazi aliyoanza leo mkoani Mtwara, Jaji Mkuu alisema katika mahakama za
Mwanzo mashauri hayo yanatakiwa uisha ndani ya miezi sita lakini yapo
mengine yamekaa zaidi ya miaka kumi.
Alisema kutokana na kuchelewa
kumalizika kwa mashauri haya, wakati mwingine humfanya msimamizi wa
mirathi kuendelea kunufaika na mali za marehemu wakati warithi wapo na
wanataabika kwa muda mrefu.
Jaji Mkuu amesema ametoa agizo
hilo pia kwa kuwa mashauri ya aina hiyo huweza kuzalisha migogoro mingi
katika jamii na kusababisha haki kutokupatikana kwa wakati.
Akizungumzia changamoto nyingine
zinazoikabili Mahakama ya Tanzania katika kutekeleza jukumu lake la
msingi la utoaji wa haki, Prof. Juma alisema Mahakama inakabiliwa na
changamoto kubwa ya wananchi kutofahamu taratibu za kisheria jambo
linalosababisha washindwe kupata haki kwa wakati.
Alisema hivi sasa Mahakama ya
Tanzania imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya
taratibu za kisheria kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Mahakamani ili
kuwasaidia wanannchi kutambua nini cha kufanya
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama
imeamua kuwa wazi katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni moja ya hatua
muhimu za mapambano dhidi ya rushwa ndani ya Mhimili huo.
Awali akizungumza na Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, Jaji Mkuu aliwaomba wakuu wa mikoa na
wakuu wa wilaya nchini kushirikiana na Mahakama ya Tanzania katika
kuwaelimisha wananchi taratibu za mchakato wa upatikanaji wa haki.
Alisema Mahakama inachangia
utulivu na Amani katika nchi pale inapotekeleza jukumu lake la msingi la
utoaji wa haki kwa wakati na endepo Mahakama haitafanya kazi yake
vizuri ni wazi itatoweka. Aliongeza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya
mwaka 2025 pia imetoa mwelekeo wa Amani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.
Gelasius Byakanwa akimkaribisha Jaji Mkuu Ofisini kwake alisema Serikali
kupitia Mkoa wake inashirikiana vizuri na Mahakama katika kuwahudumia
wananchi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.
Wakati huo huo, Mtendaji wa
Mahakama ya Rufani ya Tanzania Bwn. Solanus Nyimbi ili kutatua
changamoto ya uchakavu na ukosefu wa miundombinu ya Mahakama hususan
majengo, Mhimili huo umeandaa Mpango Kabambe wa ujenzi uliozingatia
maeneo yanayotakiwa kujengwa majengo mapya ya Mahakama, pamoja na
yanayotakiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Alisema hivi sasa majengo
yanayoendelea kujengwa ni pamoja na Mahakama za Mwanzo 22, Mahakama za
Wilaya 20, Mahakama za Mikoa (Hakimu Mkazi) 8 pamoja na Mahakama kuu 2,
zinazojengwa katika mikoa ya Mara na Kigoma.
Alisema wilaya ya Tandahimba nayo
iko kwenye mpango wa kupatiwa jengo litakalojumuisha mahakama ya Wilaya
pamoja na Mahakama moja ya Mwanzo. Aliongeza kuwa lengo ni kuwa na
Mahakama katika kila makao makuu ya Tarafa.
Bwn. Nyimbi alisema ifikapo mwaka
2021 wilaya zote zisizo na majengo ya Mahakama zitakuwa tayari
zimepatiwa majengo hayo ambapo ujenzi huo utatumia fedda za ndani pamoja
na za Benki ya Dunia.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake
ya kikazi aliyoianza leo katika mkoa wa Mtwara. Alitembelea Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara pamoja na Mahakama ya wilaya ya
Tandahimba ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi.
No comments:
Post a Comment