Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAZIRI wa TAMISEMI, Selemani
Jafo ameziagiza halmashauri zote zilizopatiwa fedha za kujenga hospitali
ya wilaya mpya, kuhakikisha wanasimamia majengo hayo yanakamilika
ifikapo June 30 mwaka huu.
Aidha ameelekeza watalaamu wa
halmashauri hizo wasimamie ubora wa majengo yanayoboreshwa na kupanua
vituo vya afya ili yaweze kudumu kwa kipindi kirefu kijacho .
Pamoja na hayo Jafo
ameridhishwa na utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa halmashauri ya
Kibaha Vijijini, mkoani Pwani miezi michache iliyopita kuhusu kukarabati
chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha Mlandizi.
Akitembelea ujenzi wa upanuzi wa
kituo cha afya Mlandizi na hospitali ya wilaya inayojengwa Kibaha
Vijijini, Jafo alitaka hospital hizo zikamilike kwa muda huo na kwa
kiwango chenye ubora kulingana na thamani iliyotolewa.
Alisema serikali imetoa kiasi cha sh. milioni 400-500 kwa vituo vya afya 97 nchini ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Jafo pia aliyaasa mashirika
yasiyo ya kiserikali ikiwemo TACAIDS kukabidhi fedha za miradi
wanayotaka kuyajenga ikiwemo maabara katika kituo cha afya Mlandizi kwa
halmashauri ya Kibaha Vijijini badala ya kusimamia wenyewe ili kuondoa
mkanganyiko.
“Kwanini mkandarasi wamlete wao,
nyie wenyewe mmeweza kujenga kwa umakini na kutumia fedha vizuri
kuboresha kituo hiki cha afya, kwanini wao wasitoe hizo milioni 600
kwenu mkasimamia miradi hiyo “

“Msije kuingizwa mkenge simamie na wanapaswa kupitisha fedha hizo kwenu “alifafanua Jafo.
Kuhusu chumba cha kuhifadhia
maiti amepongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo lake kwa asilimia
100. Nae mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa alimuomba waziri huyo
kuwaongezea fedha kwa ajili ya kuboresha zahanati ya Dutumi na Kwala.
Jafo alisema serikali itaangalia uwezekano wa jambo hilo ukizingatia Kwala kunajengwa bandari kavu hivyo ni bora huduma za kijamii zikaangaliwa.

No comments:
Post a Comment