Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua ujenzi wa ofisi za wizara
anayoiongoza zinazojengwa katika mji wa serikali uliopo eneo la Ihumwa
jijini Ddodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata taarifa ya maendeleo ya ujenzi
wa ofisi za wizara kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi Kamishna Masaidizi
Aron Lunyungu kutoka Shirika la Magereza.
Muonekano wa hatua ya ujenzi wa
ofisi za wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinazojengwa katika mji
wa Serikali uliopo eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
……………………
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua ya
ujenzi wa ofisi mpya za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
zinazojengwa kwenye
Mji wa serikali Ihumwa, mkoani Dodoma na kusema kuwa
ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Waziri Ndalichako amesema
kukamilika kwa ofisi hizo utasaidia utendaji kazi kuimarika kwa kuwa
mazingira ya kufanyia kazi yanakuwa ni mazuri zaidi.
“Ofisi kwa ujumla ni nzuri
zimejengwa vizuri naamini hata watumishi watakuwa na ari ya kufanya kazi
kwa kuwa mazingira yatakuwa bora zaidi.” alisema Waziri Ndalichako.
Waziri Ndalichako pia amemtaka
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo kuhakikisha anasimamia
kwa ukaribu ujenzi wa jengo pacha la wizara ili liweze kukamilika kwa
wakati.
Naye Msimamizi wa ujenzi huo
Kamishna Msaidizi Aron Lunyungu kutoka Shirika la Magereza amesema
ujenzi umefikia katika hatua ya ukamilishaji na kwamba wanatarajia
kukabidhi Jengo la Wizara baada ya wiki mbili kuanzi leo.
Ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia katika mji mpya wa serikali ulianza Desemba 10, 2018.
No comments:
Post a Comment