Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maemdeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.
Zainab Chaula akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa
wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania
(TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi
ya Malawi leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam..
Rose Shija kutoka WHO
akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa wataalam wa
udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Wakala wa
Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi ya Malawi leo
kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Dk Candida Shirima Kaimu
Mkurugenzi TFDA akitoa neno kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku tano kwa
wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania
(TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi
ya Malawi leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Said Abood Mjumbe wa Bodi TFDA akitoa shukurai zake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maemdeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula baada ya kufungua mafunzo hayo.
Dk Alireza Khadem Broojerdi
kutoka WHO akitoa mada katika mafunzo ya siku tano kwa wataalam wa
udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maemdeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula wa pili kutoka kushoto akiandika baadhi ya mambo wakati wa mafunzo hayo .
Dk Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO kulia akiwa na baadhi ya wakufunzi wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maemdeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maemdeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo
………………………………………………………………….
Na WAMJW- Dar es Salaam
TANZANIA yatajwa miongoni mwa
nchi 50 kati ya 194 duniani zenye mifumo imara na madhubuti ya udhibiti
wa ubora wa bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.
Zainab Chaula leo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano kwa
wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania
(TFDA), Wakala wa Chakula,
Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi
ya Malawi.
Mafunzo hayo maalum
yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-Tanzania) kwa lengo la
kuwaongezea mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuimarisha nchi hizo
kuongeza nguvu ya udhibiti wa bidhaa hizo.
“WHO imetutambua na imetupa
level (daraja) la tatu, hii ni hatua nzuri, TFDA imefanya kazi kubwa,
hii inamaanisha mifumo ya udhibiti tanzania inatambulika duniani kote na
kwamba misingi ya udhibiti ya mamlaka yetu imefikia ngazi ya
kimataifa”. Amesema Dkt. Chaula na kuongeza “Lakini pamoja na hatua hiyo
lazima iendelee kujiimarisha ili ikiwezekana tupande daraja tufikie
level 4 ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi”.
“Ili tuweze kuhakikisha
tunafanya vizuri zaidi, mamlaka yetu inapaswa kutengeneza mifumo ya
ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kuanzia viwandani hadi kwa
mtumiaji, ili kuhakikisha hakuna dawa bandia zinaingia nchini mwetu”.
Akiwasilisha mada Dkt.
Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO amesema ili kuongeza nguvu ya
udhibiti nchi zinapaswa kushirikiana kwa ukaribu.
“Tunayo malengo 17 ya kidunia
(SDGs), lengo namba tatu linasisitiza juu ya afya bora kwa wote, tunayo
pia malengo ya mwaka 2019- 2030, mpaka sasa nchi 50 ikiwamo Tanzania
sawa na asilimia 26 zimefikia daraja la tatu na nne. Nchi 45 sawa na
asilimia 23 zipo daraja la pili, nchi 96 zimefikia daraja la kwanza na
zingine zilizobaki bado hazijafikia viwango hivyo,” amesema Dkt.
Khademu.
Awali akizungumza Kaimu
Mkurugenzi wa TFDA, Dkt. Candida Shirima amesema kupitia semina hiyo
iliyoandaliwa na WHO watajifunza mbinu mbalimbali zitakazowasaidia
kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuendelea kuimarisha mifumo
ya udhibiti wa bidhaa hizo.
No comments:
Post a Comment