NJOMBE
Jeshi la polisi mkoani Njombe
limewafikisha mahakamani watu saba kwa tuhuma za kuhisishwa na mauaji ya
watoto nane yaliyoanza kutekelezwa tangu desemba 2018 akiwemo mtoto
mwenye umri wa miaka 15 anaefahamika kwa jina la DAVID KASILA anaedaiwa
kuhusika na mauaji ya watoto watatu wa familia tofauti katika nyakati
tofauti.
Watu wengine ambao uchunguzi wa
awali umebainisha kuhusika na kufikishwa mahakamani ni pamoja na Jeol
Nziku ,Nasson Kaduma na Alphonce Edward ambao wametekeleza mauaji ya
watoto watatu wa familia moja, huku wengine wakiwa ni Maliana Malekela
,Edwini Malekela na Karitus Malekela ambao wanadaiwa kuhusika na mauaji
ya mtoto Rachel Malekela.
Akizungumza na vyombo vya habari
kamanda wa mkoa wa Njombe Rennata Mzinga amesema jeshi liliwakamata na
kuwahoji watu 49 kuhusiana na mauaji hayo na kudai kwamba katika idadi
hiyo saba ndiyo waliobainika kuhusika na mauaji hayo kwa sababu
mbalimbali ikiwemo visasi, ugomvi wa mashamba pamoja na ramri
chonganishwi ambapo katika kudhibiti ukatili huo jeshi liliwakamata na
kuwahoji baadhi ya waganga, wafanyabishara na baadhi ya wanafamilia
walio uliwa wapendwa wao.
Mbali na kuwafikisha watu saba
mahakamani ,jeshi limeendelea na mchakato wa kuwabaini wahusika wengine
huku likitoa rai kwa wananchi kutuma jumbe za kweli kituo cha polisi
kuhusu wanaohusika na matukio hayo kwa kuwa kumekuwa na baadhi ya
wananchi wanatuma jumbe za uongo hatua ambayo inaleta athari
kiuchunguzi.
Watoto 8 wameuwawa njombe tangu mauaji ya watoto yaanze kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment