Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa akikata utepe kufungua Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji
ya Wazee na Vikongwe Nchini leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
mwaka wa kiutendaji wa wataalamu wa Ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti
za mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa akiongea na mtaalamu wa kutengeneza baiskeli ya miguu mitatu ya
walemavu ambaye pia ni mlemavu leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa wataalamu wa Ustawi wa Jamii
kutoka Sekretarieti za mkoa na Mamlaka za Mitaa. Waziri Mkuu ameelekezwa
kutengenezewa baiskeli moja.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la REPSS
Bi.Edwick Mapalala alipotembelea banda la maonesgho la Shirika hilo
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa wataalamu wa
ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti za mkoa na Mamlaka za Mitaa. Waziri
Mkuu ameagiza kutengenezewa baiskeli moja.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
C-SEMA Bw. Michael Marwa baada ya kutembelea banda la maonesho la
shirika hilo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa
wataalamu wa ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti za mkoa na Mamlaka za
Mitaa. Waziri Mkuu ametoa agizo kutengenezewa baiskeli moja.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
…………………….
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa amewaagiza Mawaziri wa Afya na TAMISEMI kukutana ili kupitia
upya muundo wa Kada ya Ustawi wa Jamii Nchini ili uendane na
mahitaji
ya utoaji huduma za Ustawi wa Jamii Nchini na kuitaka Wizara husika
kuhakikisha inakamilika kazi hiyo mapema.
Amesisitiza kuwa Serikali inataka
kila Sekta kuchangia katika Maendeleo ya Nchi hivyo kuwataka viongozi wa
Wizara zote mbili kuharakisha mapendekezo ya muundo huo ili kuharakisha
kasi ya maendeleo na kuwataka kumpatia majibu ya kasi hiyo haraka
iwezekanavyo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema hayo wakati wa kufungua mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa
wataalamu wa ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti za mkoa na Mamlaka za
Mitaa leo mjini Dodoma.
Aidha Waziri Mkuu amezitaka
Sekretarieti za Mkoa na Mamlaka za Mitaa kote nchini kuhakikisha
wataalamu wa Kada ya Ustawi wa Jamii wanaanza kuingia katika vikao vya
managementi ili masuala ya Ustawi wa Jamii yapewa kipaumbele lakini pia
kuitaka TAMISEMI kuhakikisha kazi zao zinaingizwa katika mipango ya
bajeti.
Aidha Waziri Mkuu amewataka
Maafisa hao kutumia vyema Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, Sheria ya Ndoa
ya mwaka 1971 na Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2010 pamoja na
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu ya Mwaka
2008 ili kuwarejeshea wananchi utu wao pale ambapo kuna dalili za
kupoteza haki zao kwa kukosa huduma stahiki.
Aidha amezitaka Halmashauri zote
chini kuendelea kuhainisha mahitaji sambamba na kuomba vibali vya ajira
za Watumishi wa Kada za Ustawi wa Jamii ili kukabiliana na upungufu wa
watumishi wa kada hiyo katika ngazi za Wilaya na Mikoa baada ya Maafisa
hao kumuomba kufanya hivyo katika maombi yao.
Wakati huo Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
katika hotuba yake fupi kwa mgeni rasmi amesema Wizara yake iko katika
hatua nzuri ya kuufanyia marekebisho muundo wa Maafisa wa Ustawi wa
Jamii Nchini lakini pia kutayarisha Sheria ya Ustawi wa Jamii pamoja na
kuundwa kwa baraza la taaluma la wataalamu wa Ustawi wa Jamii Nchini.
Aidha amemwabia Waziri Mkuu
Majaliwa kuwa Wizara yake ndiyo yenye jukumu la kutoa huduma kwa makundi
yenye mahitaji maalum ya wazee, watoto na watu wenye ulemavu hivyo
kuwakumbusha maafisa ustawi wa Jamii kuwa wanakazi kubwa ya kuhakikisha
wanatoa huduma stahiki kwa walengwa.
Aidha Dkt. Ndugulile alimwambia
Waziri Mkuu kuwa Serikali kwa sasa inatoa mikopo kwa walemavu kwa
kutumia asilimia 2 ya mapato ya ndani ya Halmashauri tofauti na awali
ambapo mikopo hiyo ikuwa kwa akina mama na vijana pekee ambapo fedha
hiyo ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri.
Dkt Ndugulile pia alisema
kumekuwepo ongezeko la vituo vya kulelea watoto laki ni kuna baadhi ya
watumishi wa vituo hivyo ambao sio waaminifu kwani wale wasio waaminifu
wanatumia watoto hao kwa kuwatumikisha kingono, kuwafanyisha kazi za
utumwa, lakini pia kuwageuza ombaomba hivyo kuwataka maafisa ustawi wa
jamii kuchunguza na kufunga vituo vyote vinavyofanya kinyume cha sheria.
Kwa mantiki amewaagiza Maafisa
ustawi wa Jamii kuhakikisha wanafuatilia utendaji wa vituo vya kulele
watoto wanasajiliwa na mamlaka husika lakini pia vianatoa taarifa ya
robo mwaka, nusu mwaka na mwaka kwa maafisa ustawi wa Jamii wa Wilaya na
Halmashauri zote Nchini.
Mkutano wa Mkuu wa mwaka wa
kiutendaji wa wataalamu wa ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti za mkoa
na Mamlaka za Mitaa wanakutana Dodoma kwa Siku tatu kwa lengo la
kukumbushana kuhusu utendaji kazi wao lakinni pia maadili yao kazi na
namna bora kudumisha kazi za ustawi wa Jamii Nchini.
No comments:
Post a Comment