NJOMBE
Ikiwa siku moja imepita tangu
naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP Siro kutuma kikosi
maalumu cha kiintelinsia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na
wauaji wilayani Njombe , Hatimae hii leo kikosi hicho kimewasili mkoani
Njombe kikiongozwa na Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la
polisi nchini Nsato Marijani.
Akizungumza katika mkutano wa
dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Njombe mkuu wa
mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka wakati akitamburisha kikosi hicho
kilichosheheni wataalamu mbalimbali kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi
na usalama nchini amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini
wahusika wamaovu hayo huku akidai hakuna mtu atakae achwa salama kama
amehusika na mauaji.
Katika mkutano huo pia
Olesendeka amemuagiza kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RPC Rennata
Mzinga kumkamata mara moja aliyekuwa mratibu wa tiba mbadala na asilia
mkoa wa Njombe Matias Gambishi ambaye pia ni afisa afya wa mkoa huo
baada ya kulalamikiwa na waganga wataalamu wa tiba asili na mbadala kuwa
amekuwa chanzo cha kusababisha migogoro katika chama chao pamoja
kufanya usajiri holela wa waganga hao.
Nae kamanda wa kikosi hicho
maalumu Nsato Marijani ambaye Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi
la polisi nchini anapata wasaha wa kuzungumza na wananchi ambapo anasema
kikosi hicho kimekuja kwa kazi ya kuwasaka wahusika wa mauaji na kwamba
kitawasaka popote walipo kwa heri ama shari.
Kwa upande wananchi wanapongeza
serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo hivyo
vya ukatili dhidi ya watoto.
No comments:
Post a Comment