Pages

Thursday, January 31, 2019

Fahamu umuhimu wa mikataba ya huduma kwa wateja


HakiPensheni


Tokeo la picha la sanlam wilson mnzava tanzania
Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha Sanlam, Wilson Mnzava (kulia), akikabidhiwa mkataba wa Bima ya Elimu wa "Sanlam Education care" wakati wa uzinduzi wake siku za nyuma
Na Christian Gaya, majira Ijumaa, Februari 01, 2019   www.majira.co.tz
Unafikiri kwa nini kuna umuhimu mkubwa kwa kampuni za bima nchini, kuwekea maanani makubwa sana juu ya utoaji wa huduma bora kwa wateja wao. Kwa sasa kampuni na taasisi nyingi zinaendeshwa kwenye mazingira ya ushindani. mkubwa ambao kila siku unaongezeka. Na ushindani huu ni wa kimataifa na wakati huo huo na masoko ulimwenguni... yanaendelea kuongezeka kila siku.

Leo gharama za kumpata mteja mpya mara nyingi zinazidi hata gharama za kumbakiza mteja wa siku nyingi. Mteja aliyeridhika na huduma huwa habishani na bei za huduma au bidhaa unazotoza na kwa maana hiyo kunakuwepo na shughuli au kazi ndogo sana za kufanya masoko na za uuzaji za kumhudumia mteja wa namna hii kuliko utekelezaji au shughuli ambazo ungefanya kwa kumtafuta mteja mpya.
Matokeo yake kwa sasa wakati wa teknolojia na habari na mawasiliano shughuli za biashara zaidi humgusa mteja. Kwa kuongezeka kwa ushindani bima nchini zinahitaji kuunganishwa na aina zote za mitandao ili kuboresha mawasiliano na hatimaye kumridhisha mteja.
Makampuni ya bima lazima ziweke malengo na mikakati ya rasilimali zao kwa nguvu zote kwa ajili ya kuwalenga na kuwabakisha wateja bora na wanaovutia na kuhakikisha ya kuwa wanapanua msingi wa wateja ambao wataleta faida kubwa ndani ya biashara ya bima hasa kwa kuwakatia bima mbalimbali na kukusanya tozo itakayotunisha kampuni ya bima kwa muda mrefu ili kutimiza ahadi za wateja wao wa muda mrefu na ya muda mfupi.
Faida kubwa kwa mteja kama atapatiwa huduma bora anakuwa amezoea na huduma ya hali juu kwa kuridhika na kiwango cha huduma na jinsi kampuni ya bima inavyomjali.
Matokeo yake ni kwamba mteja anakuwa hana muda wa kuhangaika wa kutafuta kampuni nyingine ya bima wa kuhamia wa kumpatia huduma bora zaidi hiyo anayopata. Gharama au bei ya huduma au bidhaa  siyo kwa kila kitu, mteja anabaki kuwa mwaminifu wa kampuni ya bima inayomridhisha na huduma anazotaka hata kama kutatokea na kampuni ya bima nyingine inayotoa huduma na bidhaa zinazofanana na kwa bei au gharama za chini.
Na faida kubwa kwa kampuni kwa kutoa huduma bora na hali ya juu ya kumjali mteja ni kwamba mteja aliyeridhika mara nyingi ni mtu ambaye atabaki kuwa mteja wake. Na jinsi ya kumpata mteja mpya kwa kawaida ni gharama za hali ya juu sana kuliko kumtunza na kumbakiza mteja uliyekuwa nawe tangia muda mrefu.
Hivyo kampuni za bima nchini zinatakiwa kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta ufanisi na tija katika shughuli za ulipaji wa madai mbalimbali ya wateja wao.
Hivyo ni muhimu kwa kila kampuni ya bima kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta tija na ufanisi katika shughuli za ulipaji madai. Na ili waweze  kulibainisha hili, kwa kila kampuni ya bima ni muhimu kujiwekea mapatano ya utoaji wa huduma baina yake na mteja kwa kuanzisha mkataba wa huduma kwa wateja.
Mikataba kama hii ya mapatano itakuwa ni hatua muhimu sana katika utoaji wa huduma bora katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.
Kwa kufanya hivyo wateja wa kampuni za bima watapata uhuru na uelewa wa kufahamu matarajio yake katika huduma fulani na hasa viwango vya muda ambavyo vitamwezesha mteja kupanga mambo yake vyema badala ya kusubiri huduma bila kufahamu upatikaji wa huduma hizo na kwa viwango vipi.
Kwa mfano kutokana na meneja mkuu wa bima ya maisha wa Sanlam bwana Wilson Mnzava anasema kama Sanlam wao tayari wamesha jiwekea mapatano ya utoaji wa huduma baina yao na mteja kwa kuanzisha mkataba wa huduma kwa wateja.
Anasema mapatano haya yanamwezesha mteja wao kufahamu huduma za Sanlam, viwango vya huduma na hatua atakazoweza kuzichukua iwapo viwango vya huduma vitakuwa kinyume na matarajio ya mkataba.
“Hata hivyo, ili Sanlam iweze kutoa huduma bora kwa wakati kama ilivyokusudiwa katika mapatano haya, tunategemea zaidi kupata mwitikio na ushirikiano kutoka kwa wateja ili kutimiza makubaliana haya. Mteja ndiyo kiungo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya kila siku ya kampuni yetu ya Sanlam, kwa kuwa taarifa anazotoa ndizo zinazowezesha Sanlam kama kampuni ya bima kutoa huduma stahiki” Wilson Mnzava anasema.
Mnzava anasema wana imani ya kwamba, kila mteja atatimiza wajibu wake ipasavyo ili aweze kupata huduma bora zinazotolewa kwa wakati muafaka, kwa heshima na kwa unyenyekevu. Hivyo, maoni ya mteja yatawezesha Sanlam kuongeza ubora wa huduma unazozitoa.
Bima ni mfumo wa kumwahidi kumrejeshea mwanachama hali ya afya, kipato, maisha na ustawi pindi anapopata janga au anapopoteza kitu chake cha thamani hasa ikiwa amelipia michango ya marejesho yaani premiums.
Bima hulenga kumkinga mwanachama dhidi ya janga lisilotegemewa, kwa mfano kinga dhidi ya ajali, mazishi, kulazwa hospitalini, moto, mafuriko, wizi, nk. Aghalabu, matukio hayo yasipokingwa, hurudisha nyuma maendeleo ya mtu au familia nzima kiuchumi.
Kutokana na taarifa za robo mwaka zilizotolewa na  msimamizi na mwangalizi wa bima nchini yaani TIRA kwa Septemba 2016, inaonesha kampuni ya bima ya Sanlam inaongoza nchini kwa soko la bima  ya maisha kwa asilimia 72 ikiwemo na bima ya mazishi. Taarifa hiyo pia inasema kampuni hii ya Sanlam ipo kwenye soko hili la bima zaidi ya miaka 100, na ina matawi yake zaidi ya nchi 33 duniani yakiwemo kwa bara la Afrika, Amerika, Asia, Ulaya na Australia.

No comments:

Post a Comment