Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde (wa pili kushoto) akiwasili kwenye
viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma akiwa ameambatana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard
Maboko (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda (wa
pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la
Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng
(kulia) wakielekea kutembelea kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya
kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho
ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima
Jitambue, Ishi yayonafanyika Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa
kiufundi-FP wa shirika la JHPIEGO, Bi. Lena Mfalila (kushoto) kuhusu
shughuli zinazoendeshwa na Shirika hilo kupitia mradi wa Tupange Pamoja
(TCI) ambayo ni huduma rafiki ya vijana katika afya ya uzazi kwa vijana
wakati walipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha
wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya
UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue,
Ishi yayonafanyika Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mtaalamu wa
kiufundi-AYSRH wa shirika la JHPIEGO kupitia mradi wa Tupange Pamoja
(TCI), Bw. Waziri Njau (katikati) pamoja na ‘Coacher’ -SRH wa shirika la
JHPIEGO kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI),Bi Rehema Mzungu.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa
Uzazi Salama mkoa wa Dodoma wa Shirika la PSI Tazania, Bi. Sophia Jamal
(kushoto) kuhusu elimu ya afya ya uzazi wanayotoa kwa mabinti kuanzia
miaka 13-19 yenye kauli mbiu ya Binti “Dhamiria kutimiza ndoto
yako-“Simama Imara” “Vaa Taji”, “Kua Mzuri” wakati alipotembelea kijiji
cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana
kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli
mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika
viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi
.Mwanahamisi Mukunda aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk.
Leonard Maboko wakipata maelezo kutoka kwa Bi. Debora Frank (kushoto)
ambaye ni Afisa Miradi wa Huduma za Vijana wa shirika la EGPAF ambao
wanaotekeleza mradi wa USAID wa Boresha Afya kwa kushirikiana na
ENGENDER Health kuimarisha afya za watanzania wote na kuongeza
upatikanaji wa huduma za afya timilifu za kiwango cha juu na jumuishi
wakati alipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki
ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI
Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi
yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Mradi unaolenga
kuboresha huduma za kinga na matibabu ya VVU/UKIMWI, uzazi wa mpango,
Kifua Kikuu na kutoa huduma mahususi wa kuyafikia makundi maalum kwa
watoto na vijana.
Pichani
ni Hawa Musa (20) mmoja kati ya vijana zaidi ya 2000 wanaonufaika na
mafunzo ya ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Shirika la EGPAF ambapo
mafunzo hayo yamewasiaida kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo vikoi,
mikoba ya shanga, Ubuyu, sabuni za maji na miche ambazo zinawasaidia
kupata fedha za matumizi mbalimbali akishiriki kuonyesha kazi zake
katika mabanda ya kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki
ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI
Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi
yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Meneja masoko
wa Shirika lisilo la kiserikali la T-MARC Tanzania, Bi. Sophia Komba
kuhusu shirika hilo linalotoa elimu kuhusu matumizi ya Kondomu ili
kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwa pamoja na UKIMWI
katika mabanda ya kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki
ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI
Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi
iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. T-MARC Tanzania
wanafanya kazi kwa kushirkiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto katika kuboresha afya ya jamii ya watanzania
ambapo pia ni wasambazaji wa bidhaa za afya ambazo ni Kondomu ya kiume-
Dume, Kondomu ya kike Lady Pepeta na vidonge vya uzazi wa mpango-Flexi
P. Wa pili kushoto ni Outreach Educator wa T-MARC Tanzania, Dotto Iddy.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, Mkuu wa Wilaya
ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda pamoja na Mkurugenzi Mkazi na
Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa
(UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri
mwandamizi wa masuala ya afya ya uzazi kwa vijana kutoka mradi wa Sauti
unaratibiwa na Shirika la JHPIEGO, Esther Majani (wa kwanza kushoto)
kuhusu shughuli wanazofanya za kutoa elimu ya kupunguza maambukizi mapya
ya VVU kwa makundi hatarishi ikiwemo mabinti walio nje ya shule wa
miaka 15-24 wakati walipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya
kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho
ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima
Jitambue, Ishi yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Kutoka
kushoto kwenda kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Masuala ya Madawa ya Kulevya na Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa
Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi
Mukunda, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde, Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard
Maboko, Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI
la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng pamoja na Balozi wa
Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo
wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele
cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri
Jijini Dodoma.
Mkuu
wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda akizungumza jambo kwa niaba
ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge wakati
akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati
wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha
maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri
Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akihutubia wananchi wa Dodoma wakiwemo
vijana wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea
kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya
mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya
Jamhuri Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa
Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea
kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya
mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya
Jamhuri Jijini Dodoma.
Balozi
wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo
akizungumza na hadhira ya vijana (hawapo pichani) wakati wa hafla ya
kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima
Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Madawa ya Kulevya na Ukimwi
ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa akitoa salamu za
kamati yake wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana
kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli
mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika
viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard
Maboko akitoa neno kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde
wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele
cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri
Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard
Maboko akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la
Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng
wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele
cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri
Jijini Dodoma.
Balozi
wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la
Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng
wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele
cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri
Jijini Dodoma.
Msanii
wa Bongo Flava Maua Sama akitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma wakati wa
hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha
maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri
Jijini Dodoma.
Mchekeshaji
maarufu nchini Stan Bakora akitoa burudani ya kuhamasisha upimaji wa
UKIMWI kwa njia ya vichekesho wakati wa hafla ya kufunga wiki ya
shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI
Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi
iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Afisa
Maendeleo Vijana wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Tumsifu Mwasambale (kushoto)
akionyesha moja ya picha iliyoshinda wakati wa wiki ya shughuli za
kijiji cha vijana iliyochorwa kijana Edward Malongo na kupigwa mnada
ambapo zaidi shilingi 2.7 zilipatikana ambapo nusu zilienda kwa mchoraji
na nyingine kwenye mfuko wa udhibiti wa Ukimwi (ATF) wakati wa hafla ya
kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima
Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa
kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira ya vijana walio nje ya shule ya
Panama, Bw. Dunia Salumu wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za
vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika
viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa
kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Vijana Queens, Ngesa
Selemani wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea
kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya
mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya
Jamhuri Jijini Dodoma.
Baadhi
ya kazi za mshindi wa kwanza katika eneo la uchoraji Edward Malongo
(tisheti nyeupe) wa picha zinatoa ujumbe wa kuhamasisha kampeni ya
kutokomeza VVU zikionyeshwa kwa wageni wa meza kuu wakati wa hafla ya
kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima
Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Baadhi
ya wakazi wa Dodoma walioshiriki hafla ya kufunga wiki ya shughuli za
vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika
viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi
Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa
Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng amesema kuwa kuwa shirika hilo
litaendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa
huo.
Akizungumza
jana Jijini Dodoma wakati wa kilele cha shughuli za vijana kuelekea
maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Dk Zekeng alisema kwamba kuna
haja kubwa ya kuhakikisha kwamba taifa linapambana na maambukizi mapya
kwa kuhakikisha kwamba kunatolewa huduma rafiki miongoni mwa vijana
ambao ndio kundi kubwa linalohitaji msaada kwa sasa ni jukumu la kila
mwanajamii na kuomba ushirikiano wadau wote katika mapambano hayo.
Alisema
wakati taifa nusu yake ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 na huku
takwimu zikionesha kwamba kundi hilo linaathirika sana ipo kila sababu
ya kutengeneza mkakati na kuweka mazingira rafiki ili kuokoa kizazi
hicho.
Alisema
kwa sasa vijana wanahitaji kusaidiwa kwa kuwaweka katika mazingira
rafiki ya kuhitaji huduma zinazotolewa katika kampeni ya kukabiliana na
maambukzi ya VVU.
Alisema
kwa sasa huduma hizo si rafiki ziko chache na hivyo kuwafanya vijana
wasishiriki kwa sababu ya hofu ya kunyanyapaliwa na pia kukosekana kwa
elimu hitajika.
Aliongeza
ili taifa lifikie uchumi wa kati unaotakiwa mwaka 2025 na kufikia
agenda 2030 ni lazima liwe ni taifa lenye vijana wanaojitambua na wenye
afya bora.
“iko
haja ya kushawishi vijana ambao ndio kundi kubwa kujitambua na katika
package nzima wajue namna ya kujikinga, na kuishi kwa afya hata kama
wana virusi” alisema Dk Zekeng na kusisitiza kwamba shirika lake
litaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba vijana
wanapatiwa elimu ya kutosha na mahitaji mengine katika vita dhidi ya
UKIMWI.
Alibanisha
kuwa takribani watu milioni 37 Duniani wanaishi na Virusi vya UKIMWI na
sehemu kubwa wakiwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Siku
ya UKIMWI Duniani huadhimishwa kila ifikapo Disemba Mosi kila mwaka
ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi ambapo mwaka
huu yanafanyika Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Warizi
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
No comments:
Post a Comment