Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya
Teknolojia Bora ya Uzalishaji wa Dhahabu , Mkoani Geita
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitembelea baadhi ya mabanda wakati
wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya Teknolojia Bora ya Uzalishaji wa
Dhahabu , Mkoani Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi
Robert Gabriel akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya
Teknolojia Bora ya Uzalishaji wa Dhahabu, ambapo alisisitiza kuwa
ataendelea kusimamia rasilimali ya madini katika Mkoa wa Geita ili iweze
kuwanufaisha wakazi wa Mkoa huo na Taifa kwa Ujumla.
Waziri wa Madini Mhe. Angelah
Kairuki akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya Teknolojia
Bora ya Uzalishaji wa Dhahabu, ambapo pamoja na mambo mengine aliitaka
kampuni ya madini ya Geita Gold Mine kuwafidia wananchi waliothiriwa
nyumba zao mitetemo ya uchimbaji wa madini, kufikia Oktoba 24, 2018
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa hafla ya ufungaji
wa Maonesho ya Teknolojia Bora ya Uzalishaji wa Dhahabu, ambapo pamoja
na mambo mengine aliziasa benki za kibiashara kushiriki katika ukuaji wa
sekta ya madini kwa kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo, lengo
likiwa ni kuwasaidia wachimbaji hao kuwa na masoko ya uhakika wa
madini.
No comments:
Post a Comment