Wasanii wa kundi la Wanne Star
wakicheza ngoma za utamaduni jukwaani wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo
leo Oktoba mosi, Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa
Shirikisho la vyama vya Wadau wa Utalii Tanzania, Bwana Abdukadir Luta
Mohamed (Katikati) akiwa kwenye meza kuu wakati wa tamasha hilo.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Kitaifa, Profesa Audax Mabula
akizungumza katika ufunguzi huo ambapo amesema Tanzania inajivunia kuwa
na Lugha kuu nne zilizopo Barani Afrika. Wakati wa ufunguzi huo leo
Oktoba Mosi katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Tanzania ni
ya pili kwa Urithi wa Maliasili baada ya Taifa la Brazil la Bara la
Amerika ya Kusini kwa kuwa na vivutio vingi vya Asili.
Hayo yameelezwa
leo wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Urithi Wetu (Urithi
Festival) linalofanyika katika viunga vya Kijiji cha Makumbusho
Jijini Dar-es –Salaam na
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama
vya Wadau wa Utalii Tanzania, Bwana Abdukadir Luta Mohamed.
Amesema kuna
vivutio vingi vya urithi wa utamaduni, ukiweka pamoja vivutio vya
utalii wa asili na utamaduni, Tanzania inaweza kuongoza kwa kuwa na
vivutio vingi vya utalii duniani.
Bwana Mohamed amevitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa pamoja na tamaduni, makabila, mila, desturi, vyakula na Malikale.
Awali akizungumza
wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
ya Tamasha la Urithi Kitaifa, Profesa Audax Mabula ameeleza kuwa
Tanzania inajivunia kuwa na lugha kuu nne zilizopo Barani Afrika.
Amezitaja lugha
hizo kuwa ni Wabantu ambao inawajumuisha makabila kama vile Wasukuma,
Wajita na Wanyamwezi, Wanailotiki inawajumuisha Wamaasai,
Wakushitiki-inayojumuisha Wairaq,Wambulu, Wakhoisan –inayowajumuisha
Wahadzabe na Wasandawe.
Profesa Mabula
ameeleza kuwa, Kabila la Wasandawe limeanza kupotea lakini ni imani kuwa
kabila hilo litaendelezwa kupitia tamasha la Urithi Wetu.
Mwenyekiti huyo
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Kitaifa amesema “Utalii wa
Utamaduni utainuliwa kupitia Urithi festival.
Amewaomba
Watanzania kushiriki vema kwenye Tamasha hili na kuvaa mavazi ya
Kitanzania kama vitenge, ngozi, batiki, shuka na mavazi mengine ya asili
katika maadhimisho haya na ya kila Mwezi wa tamasha la Urithi.
“Urithi festival
inatoa fursa kwa watu wote. Tunapenda waje hapa waone ubunifu, vitu
muhimu na mambo ya ubunifu wa kila aina” Amesema Profesa Mabula.
Ameongeza kuwa, Watu tuheshimu Urithi wetu wa Utamaduni ili kuchochea Utalii wa ndani na nje ya Nchi.
Tamasha hilo
limepambwa na vikundi mbalimbali vya ngoma za kiasili, sarakasi,
nyimbo, Wajasiriamali, vyakula vya kiasili ikiwemo nyama choma za
porini kama swala na nyati zilnazouzwa kwa shilingi elfu Nane kwa kilo.
Naye Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard
Mayongela katika kuunga mkono Tamasha la Urithi Wetu, imekabidhi fulana
100 katika hafla hiyo.
Tamasha hilo
ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka, linaandaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii, na lilizinduliwa rasmi Septemba 15 mwaka huu jijini
Dodoma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan likiwa na lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini.
Imeelezwa kuwa,
baada ya Tamasha hilo kufungwa rasmi jijini Dar-es-Salaam litaendelea
kufanyika Jijini Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeida Karatu,
ambako ni njia kuu ya kuingilia katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na
Serengeti kuanzia Oktoba 8 hadi 13.
No comments:
Post a Comment