Pages

Wednesday, October 31, 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AKABIDHI RUZUKU YA BILIONI 1.2 KWA VIJANA WAKULIMA.

 

Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony P. Mavunde  leo Oktoba 31, 2018 amekabidhi kwa Vijana wakulima na SIDO awamu ya kwanza ya ruzuku ya jumla ya Tsh 1,200,000,000 iliyotolewa na USAID katika utekekelezaji wa mradi wa “Feed the Future” unaotarajia kuwafikia Vijana 33,000 katika mikoa ya Iringa,Mbeya na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Kata ya Kiwele,Kalenga Mkoani Iringa ambapo Mh Mavunde amechukua fursa hiyo kuwashukuru USAID kwa namna wanavyosaidiana na serikali kutatua changamoto zinazoakabili vijana na kutumia fursa kuwataka Vijana nchi nzima kushiriki kwenye sekta ya Kilimo na kuahidi kwamba serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kilimo ili vijana wengi  zaidi waweze kunufaika.

Wakuu wa Wilaya za Kilolo na Mbeya,kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Iringa na Mbeya,*Mh Asia Abdallah* na Mh Paul Ntinika wameahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa program hii na kuhakikisha kwamba malengo ya program hii yanafikiwa na vijana wengi zaidi kunufaika.

Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi wa Uchumi wa USAID Bi Terhi Majanen ameeleza kwamba ruzuku hiyo ya awamu ya kwanza inalenga kwenda kuzalisha ajira 735 na uanzishwaji wa viwanda vidogo 200.




No comments:

Post a Comment