Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
imekabidhi rasmi majukumu kwa Balozi wa Hiari wa Utalii Bi Bi Judith
Raymond Mushi aliyepewa jukumu la kufanya kazi na TTB ya kuvitangaza
vivutio vya Tanzania katika nchi ya Italia. Bi. Judith ambaye ni
Mtanzania, anafanya kazi ya
kufundisha Lugha ya Kiswahili nchini
Italia.
Wakati wa makabidhiano hayo
yaliyofanyika Septemba 27, 2018 katika ofisi za TTB jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa TTB Bi. Devota Mdachi amemkabidhi rasmi sharia na
taratibu zinatakiwa kufuatwa wakati anatekeleza jukumu hilo kupitia
matukio mbalimbali atakayokuwa anahudhuria akiwa italia.
Pamoja na msaafu huo Bi . Judy
alikabidhiwa majarida yenye taarifa za utalii wa Tanzania yanayotumiwa
kama nyenzo ya kutangazia utalii wa Tanzania katika masoko mbalimbali ya
Utalii Duniani.
TTB imeweka utaratibu maalumu wa kuwapata mabalozi wa hiari wa Utalii.
No comments:
Post a Comment