Pages

Sunday, September 30, 2018

MATUKIO MBALIMBALI YA BENKI YA NBC WIKI HII KATIKA PICHA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akikabidhi zawadi ya pikipiki  kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya mauzo iliyopewa jina la 'Mimi ni Shujaa' kwa Patrick Paul jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa wafanyakazi wa benki hiyo ina lengo la kuhamasisha utendaji kwa wafanyakazi wanohusika katika kitengo cha mauzo ndani ya benki hiyo. Wanaoangalia kutoka wa pili kushoto ni,  Kaimu Mkurugenzi  wa  Wateja Binafsi, Andrew Lyimo, na Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Wateja Binafasi wa Absa Group, Nazim Mahmood.
  Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Andrew Lyimo, akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi wafanyakazi bora wa kampeni ya mauzo iliyopewa jina la ‘Mimi ni Shujaa’ ya benki hiyo hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia) pamoja na ujumbe wake wakimsikiliza   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Taifa la  Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw.William Erio (kushoto), walipotembelea ofisini kwake, Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo yenye lengo la  kukuza mahusiano yao ya kibiashara.
Ofisa Mtendaji Mkuu Wateja Binafsi  wa ABSA Group,  Vimal Kumar (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa pili kulia) huku Mkuu Mkuu wa kitengo  cha Uhai wa Wateja wa benki hiyo, Gaudence Shawa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Andrew Lyimo wakiangalia katika hafla ya kuwakabidhi zawadi wafanyakazi bora wa kampeni ya mauzo iliyopewa jina la ‘Mimi ni Shujaa’ ya benki hiyo.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akishikana mikono na   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’I Issa wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakimtembelea ofisini kwake na kuzungumzia fursa mbalimbali za ushirikiano  jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa tatu kushoto, mstari wa mbele), akipiga picha ya pampoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’I Issa (kulia kwake) wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakimtembelea ofisini kwake na kuzungumzia fursa mbalimbali za ushirikiano  jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment