Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.
Na Mwandishi wetu, Geita.
Mageuzi makubwa
katika sekta ya madini nchini yameifanya sekta hiyo kuendelea kuongeza
mapato ya Serikali kutoka bilioni 194.6 ilizopanga kukusanya mwaka
2017/18 hadi kufikia shilingi bilioni 301.6 ikiwa ni ongezeko la zaidi
ya asilimia 55.
Hayo yameelezwa
leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mkoani Geita wakati
akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Serikali.
Dkt. Abbasi
ameeleza kuwa ongezeko hilo la mapato katika sekta ya madini
limechagizwa na mabadilikomkatika sheria za madini, kujengwa kwa ukuta
wa Mirerani na kuzuia kwa usafirishaji wa mabaki (kaboni) ya dhahabu nje
ya mkoa yanapochimbwa madini.
“Mheshimiwa Rais
aliagiza kujengwa ukuta eneo la wachimbaji wadogo la Mirerani na April
mwaka huu ukuta huo ulikamilika na kuwezesha kuongezeka kutoka kilo
164.6 za madini ya Tanzanite yenye thamani yas milioni 71.8 mwaka 2016
hadi kufikia kilo 449.6 zenye thamani ya shilingi milioni 893.8 kwa
kipindi cha Januari hadi Juni 2018”, ameeleza Msemaji Mkuu wa Serikali.
Ameeleza kuwa
kutokana na usimamizi mzuri, makampuni ya uchimbaji madini yameendelea
kutoa mchango wake kwa jamii ambapo Geita Gold Mine imetoa shilingi
bilioni 9.2 kwa mkoa wa Geita kama mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo
ya mkoa huo.
Aidha, Msemaji
Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa zuio la kaboni zenye dhahabu
kusafirishwa na kuchakatwa nje ya mkoa zinakozalishwa limesaidia
kuongeza pato kwa Serikali kufikia shilingi milioni 850 kwa mwezi Agosti
mwaka huu kutoka shilingi milioni 400 kwa mwezi April.
Kwa mujibu wa
Msemaji wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kufanya
mageuzi mbalimbali ikiwemo kujenga vituo saba vya umahiri
vitakavyokamilika Disemba mwaka huu kwa thamani ya shikingi 11.9
kuwapatia wachimbaji wadogo mafunzo na utaalamu zaidi wa uchimbaji.
Aidha, vituo vinne vya mfano pia vitajengwa kwa thamani ya shilingi tono
kuwasaidia wachimbaji kupata teknolojia rahisi ya uchenjuaji wa madini
na kuyaongezea thamani.
Kwa upande wa
sekta ya afya, Dkt. Abbasi ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa wa vifaa,
wataalamu na majengo umefanyika katika hospitali za Muhimbili,
Mloganzila, MOI, Bugando, Benjamin Mkapa na ambapo hivi sasa Tanzania
inapokea wagonjwa kutoka Komoro, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia kwa ajili ya kupata matibabu
ya kibingwa ya moyo, figo, mifupa na kuongeza uwezo wa kusikia.
“Serikali
imeendelea kusogeza huduma za afya karibu kwa wananchi kwa kujenga
hospitali za rufaa katika mikoa saba, hospitali za Wilaya 67 zinajengwa
mwaka huu kwa gharama ya shilingi bilioni 105 na tayari vituo vya afya
210 pamoja na nyumba za wahudumu wa afya vimejengwa” amesisitiza Dkt.
Abbasi.
Katika hatua
nyingine, Dkt Abbasi ameeleza kuwa hali ya uchumi wa Tanzania umeendelea
kuwa imara ukikua kwa takribani asilimia 7.0 mpaka 7.1 kwa mwaka na
kwamba kwa mujibu wa ripoti mbalimbali ikiwemo ya World Economic Forum,
Tanzania ni ya tisa duniani kwa ukuaji wa uchumi na kwa Afrika inashika
nafasi ya tano kwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi.
Ameeleza kuwa
hali nzuri ya ukuaji wa uchumi unaifanya Serikali kuendeleza mageuzi
makubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, miundombinu, afya na
nishati ili kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo
mwaka 2025.
Miongoni mwa
mageuzi makubwa yanayoendelea nchini ni pamoja na uchezi wa miundombunu
kama reli ya kisasa ya Standard Gauge, ujenzi wa bwala kubwa la
kuzalisha umeme wa megawati 2100 kutoka bonde la mto Rufiji na hivi
karibuni ambapo Rais alizindua barabara ya Juu (Flyover) iliyopo TAZARA
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment