Pages

Saturday, September 29, 2018

Kukosa uaminifu na ukosefu wa bidhaa zisizowavutia wateja kizuizi soko la bima kutopanuka wigo


Na Christian Gaya, majira 28 Septemba 2018
Pamoja na juhudi zote za kuboresha uelewo wa umuhimu wa hitaji la kuwa na bima miongoni mwa watanzania kiwango cha wigo wa soko la bima bado kipo chini sana ingawa wadau wengi wana wanategemea ya kuwa uwingo wa watu kuwa na bima utaongezeka.


Kwa  umuhimu wa sekta ya bima kwa aina yeyote ya uchumi, hasa kama ulinzi kwa biashara na watu wenyewe kwa majanga hatarishi imekuwa ni kero sana kwa wadau na kusababisha kuwa ndiyo chanzo cha matatizo. Ingawa baadhi ya wadau wa sekta ya bima wanasema kuna maendeleo kidogo katika sekta hii. 

Kwa takwimu zilizopo inaonesha uwigo wa bima hapa nchini upo chini ya asilimia moja na mchango wake kwa pato la taifa bado uko chini pia kwa mwaka. Kwa mfano kwa mwaka unaoshia 31Desemba 2016, sekta ya bima nchini iliongezeka kwa asilimia 7.0 kutoka shilingi bilioni 618.9 fedha za Kitanzania mpaka kufikia shilingi bilioni 660.0 za Kitanzania

Uwigo huu wa soko la bima kuwa kidogo, unalalamikiwa kuchangiwa na sababu mbalimbali. Na mojawapo ya sababu kubwa zimekuwa ni kuwa na uelewo mdogo juu ya dhana nzima la bima miongoni mwa watanzania, kipato kidogo cha watanzania cha kuweza kununulia bima, utaratibu mbaya wa uendeshaji wa soko la bima, na kuwa na bidhaa za bima zisizowavutia wateja.
Na moja kubwa kabisa, kukosa nguvu ya serikali kutowekea mazingira mazuri na kipaumbele kwa biashara ya bima hivyo kufanya kama kizuizi kikuu cha ukuaji wa bima nchini.

Wauza bima kukosa uaminifu miongoni mwa idadi kubwa ya Watanzania imekuwa ni sababu mojawapo ya ukuaji mdogo wa uwigo wa biashara ya bima nchini. Taarifa zinazopatikana zinaonesha ya kuwa Watanzania wengi wanaacha kukata bima kwa sababu ya ugumu na usumbufu wa utaratibu wa madai wakati maafa hatarishi yakitokea au wakati bima yake imeshaiva tayari.

Ingawa jambo hili kwa kiasi kikubwa limeweza kuingiliwa kati na kutatuliwa kwa mshirikiano mkubwa na watoa bima na msimamizi wa bima yaani kamishna wa bima Tanzania (TIRA).
TIRA kwa upande wake kama msimamizi wa bima nchini imeweza kutumia nguvu za kisheria ilizopewa kuhakikisha ya kuwa kampuni za bima nchini zinafuata utaratibu na kanuni pamoja na sheria zilizowekwa kwa ajili ya kumlinda mlaji na kwa manufaa ya uchumi wa nchi kwa ujumla. 

Kipingamizi kikubwa cha bima hapa Tanzania hasa ni gharama ya juu ya bei ya vifurushi vya bima. Na kwa wale wanaoilalamikia Serikali kwa bima kuwa na uwingo kidogo nchini, wanasema serikali ambayo ina msingi wa rasilimali nyingi na kubwa mara nyingi inakatia bima ila inakuja kutifua kwa upande wa bei za bima na ulipaji wake.  

Utafiti unaonesha ya kuwa sekta ya bima haijaguswa kabisa, kwa sababu mpaka sasa haijatumia vizuri sekta isiyo rasmi ambayo inashikiria karibu asilimia 90 ya idadi yote ya watu wote wa hapa nchini. 

Ambayo hii ni mojawapo ya sababu kubwa ya ulazima wa kuanzisha bima kwa ajili ya kundi hili kubwa la Watanzania ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi ambao karibu wote wanafanyia kazi zao kwenye mazingira hatarishi yasiyokuwa na bima ya aina yeyote.

Kabla, wadau katika sekta hii wamekuwa wakifanya bidii kubwa ya kutaka kubadilisha mazungumzo hasi juu ya huduma za bima nchini. Na hii imekuwa ni matokeo ya kuwa na sekta nzuri ya usimamizi wa bima, angalau uelewo zaidi juu ya bima za magari unaongezeka kidogo.

Ili kuleta mabadiliko yanayoeleweka katika sekta hii ya bima, wataalamu wengi wanapendekeza baadhi ya hatua muhimu kuchukuliwa ambazo wanasema huenda zinaweza kuboresha sekta. Wanazipigia debe sana kuanzishwa kwa bima zinazolingana na mahitaji ya mteja mwenyewe kwa wakati huo, na bima ndogo kwa ajili ya watu waliopo kwenye sekta isiyo rasmi na bima ya miiko au takaful. 

Ikumbukwe ya kuwa mwendelezo wa soko la bima ndogo ndogo ni mojawapo ya malengo ya mwendelezo wa ukuzaji wa soko la bima yanayofanywa nchini, kwa malengo na mikakati ya TIRA ambapo Kamishna wa Bima alianzisha na kuungwa mkono na wadau wa sekta kama ndiyo mwanzo wa jambo wa kuanzia kuitangaza maendeleo ya sekta ya bima nchini. Inandelea wiki ijayo

No comments:

Post a Comment