Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
wakitoka kukagua mradi wa maji wa Bigwa Msongeni ulioko katika Manispaa
hiyo. Kamati ya LAAC iko ziarani Mkoani Morogoro kwa ajili ya kukagua
miradi ya maji na barabara katika inayotekelezwa katika Manispaa ya
Morogoro.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiangalia
maradi wa maji wa Bigwa Msongeni. Wajumbe hao wapo ziarani Mkoani
Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi ya maji na barabara katika
inayotekelezwa katika Manispaa ya Morogoro.
Mhandisi
wa Maji Manispaa ya Morogoro Ndugu Edward Kisalu akitoa taarifa ya
mradi wa maji wa Bigwa Msogeni mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC). Wajumbe hao wapo ziarani Mkoani Morogoro kwa
ajili ya kukagua miradi ya maji na barabara katika inayotekelezwa katika
Manispaa ya Morogoro.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
wakisaidiwa kushuka mlima kwa ajili ya kwenda kukagua mradi wa Maji wa
Bigwa Msongeni msongeni. Wajumbe hao wapo ziarani Mkoani Morogoro kwa
ajili ya kukagua miradi ya maji na barabara katika inayotekelezwa katika
Manispaa ya Morogoro.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Vedasto
Ngombale akitoa maelekezo kwa watendaji wa Manispaa ya Dodoma wakati
Kamati hiyo ilipotembelea Mradi wa maji wa Bigwa Msongeni ulioko katika
Manispaa hiyo. Kamati ya LAAC iko ziarani Mkoani Morogoro kwa ajili ya
kukagua miradi ya maji na barabara katika inayotekelezwa katika Manispaa
ya Morogoro.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
Selemani Jafo akikagua kiwanda cha kisasa cha kutengeneza matofali cha
Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Ujenzi wa Dampo la Kisasa unavyo endelea Katia Jiji la Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiongea na viongozi wa Mkoa wa Tanga pamoja na wananchi wa Mikanjuni alipotembelea kukagua ujenzi wa kituo cha afya Mikanjuni.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mkoa na Jiji la Tanga
alipotembelea Mkoani humo.
.........................................
Halmashauri ya Jiji la Tanga imepongezwa kwa kujenga miradi ya maendeleo yenye viwango vinavyoridhisha. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alipokuwa katika ziarani ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Tamisemi mkoani Tanga. Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ametembelea ujenzi wa Dampo la kisasa linalojengwa kwa Sh.Bilioni 9, uboreshaji wa kituo cha afya cha Mikanjuni kinacho gharimu sh.Milioni 400 pamoja kiwanda cha kufyatua matofali cha halmashauri ya Jiji kilichogharimu Sh.milioni 80. Katika ukaguzi wa miradi hiyo, Waziri Jafo hakuacha kumsifu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi inayojengwa kwa ubora mkubwa. Aidha, Waziri Jafo amemmwagia sifa Mkurugenzi huyo kwa ubunifu mkubwa wa kuanzisha kiwanda cha kisasa cha matofali kinachotumia teknolojia ya kisasa zaidi ambacho kinauwezo wa kufyatua matofali zaidi ya 5000 kwa siku ambapo hadi sasa wameshapata tenda ya kutengeneza matofali 100,000 kutoka kwa kampuni moja pekee huku makampuni mengine na wananchi wa kawaida wakimiminika kiwandani hapo kutaka matofali kutokana na ubora mkubwa wa matofali hayo. Waziri Jafo amewataka wakurugenzi wa halmashauri nyingine hapa nchini kuiga mfano huo mzuri wa vyanzo vya mapato ili kuziongezea mapato halmashauri zao.
No comments:
Post a Comment