NA
MWANDIHI MAALUM
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde
ameishukuru sekta binafsi kwa mchango mkubwa inaoutoa katika sekta ya Uchumi wa
Viwanda na fursa za Ajira inazozitengeneza kupitia uwekezaji.
Naibu
Waziri Mavunde ameyasema hayo katika uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji
kikali cha K-VANT katika Hotel ya Serena Jijini Dar es salaam ambapo pia
amechukua fursa hiyo kuipongeza kampuni ya MEGA BEVERAGES kwa kutoa fursa za
AJIRA kwa wananchi zaidi ya 1000 na pia kwa uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha
vinywaji na kuitaka kampuni hiyo kuzingatia ubora ili kuifanya bidhaa yao kuwa
shindani na kuvuka mipaka ya Tanzania.
Akimkaribisha
Mgeni Rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni MEGA BEVERAGES Bw. Francis Kimaro
ameishukuru Serikali kwa mazingira wezeshi yaliyofanikisha uwekezaji huo wa
kiwanda na kuahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora.
No comments:
Post a Comment