Pages

Sunday, July 22, 2018

SERIKALI YAAGIZA KUCHUNGUZWA KWA KUMBI ZA STAREHE MKAONI MARA KWA KURUHUSU WATOTO KUINGIA NA KUTUMIA POMBE.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na watendaji wa  Mkoa wa Mara alipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo kujionea utekelezaji katika sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima akimuelezea Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kuwa anaendelea kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivyo kulingana na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 na Katiba ya nchi.
Baadhi ya watendaji wakisikiliza maelekezo ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo kujionea utekelezaji katika sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii.(PICHA NA WAMJW)
Na Mwandishi Wetu Musoma Mara
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewaagiza viongozi wa Mkoa wa Mara na Wilaya ya Musoma kuchunguza tuhuma zinazohusisha kumbi za starehe wilayani Musoma Mkoani Mara kwa kuruhusu watoto walio chini ya miaka 18 kuingia na kutumia pombe ndani ya kumbi hizo.
Agizo hilo limetolewa wilayani Musoma na Naibu Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Mkoa wa Mara kwa ziara ya kikazi.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa akiwa katika ziara yake amepokea Malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai moja ya kumbi mbili za starehe  kuwaruhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kutumia pombe wakiwa ndani ya kumbi hizo.
“Niwatake uongozi wa mkoa kufuatilia suala hili kwa undani na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika katika suala hilo’’ alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Amesema kuwa kwa mujibu wa wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kinasema mtu ambaye ni mmiliki au anayeendesha au ni msimamizi wa ukumbi wa muziki, Bar, au klabu ya usiku hatamruhusu mtoto kuingia katika maeneno yao.
Kifungu kinaeleza kuwa mtu atakayekiuka kifungu hiki atakuwa ametenda kosa na atakapotiwa hatiani atalipa faini ya kiasi kisichopungua Sh Millioni moja na kisichozidi Sh Millioni tano au kifungo kisichozidi miezi 12 au vyote kwa pamoja.
Ameongeza kuwa Serikali haitavumilia kuona watoto wakishiriki katika shughuli za usiku ambazo zinatahatarisha ustawi wao nchini.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima amemuelezea Naibu Waziri kuwa anaendelea kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivyo kulingana na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 na Katiba ya nchi.
Mhe. Malima ameongeza kuwa katika mkoa wake hawataruhusu kutokea kwa matukio hayo na kwatahadharisha wamiliki wote wa kumbi za starehe kuzingatia Sheria inayomlinda mtoto.
Mhe. Malima ameeleza kuwa Serikali ya mkoa itaendelea kupambana pia na vitendo vya ukatili wa Kijinsia, Ndoa na Mimba za Utotoni ambazo zinashamiri katika mkoa huo.

No comments:

Post a Comment