Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza umuhimu wa kutumia kwa
malengo yaliyokusudiwa magari 45 yaliyotolewa na Serikali kwa wadhibiti
ubora wa Elimu ngazi ya Kanda na Wilaya leo Jijini Dodoma wakati wa
Hafla ya kukabidhi magari hayo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali
kuboresha elimu hapa nchini.katika hafla hiyo Baraza la Mitihani
Tanzania nalo lilipatiwa magari 2 na kufanya jumla ya magari
yaliyotolewa kuwa 47.
Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiendesha moja ya magari yaliyotolewa
na Serikali kwa wadhibiti ubora wa Elimu ngazi ya Kanda na Wilaya leo
Jijini kama sehemu ya kuzindua na kukabidhi magari hayo.
Sehemu ya magari 47 yalitolewa na
Serikali ambapo wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya
wamekabidhiwa magari 45 na mawili yamekabidhiwa Baraza la Mitihani
Tanzania (NECTA).
Sehemu ya washiriki wa hafla ya
kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa
wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Magari yalikabidhiwa kwa wadhibiti
ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya yakiondoka katika viwanja wa
Chuo Kikuu Dodoma baada ya hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo
Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako alikuwa mgeni rasmi.
Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza Bw. Erick Maximillian
ambaye ni mwanafunzi Bora wa masomo ya Sanaa nafasi ya pili Kitaifa
kutoka shule ya Sekondari Mvumi Dodoma wakati wa hafla kukabidhi magari
47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa
elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani
Tanzania (NECTA).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa
hafla ya ya kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45
yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2
yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora
Kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi Ufrasia Buchuma akitoa
neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako mara baada ya hafla ya kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya
magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya
Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari 47 ,
ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa
elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani
Tanzania (NECTA).
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO
……………….
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali imewataka Wadhibiti Ubora
wa Elimu katika ngazi zote kutekeleleza majukumu yao
kwa weledi ili
kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.
Akizungumza leo Jijini Dodoma
wakati wa hafla ya kukabidhi magari 47 kwa wadhibiti Ubora wa Elimu na
Baraza la Mitihani (NECTA), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako amesema ku ni utekelezaji wa sehemu ya mikakakti
ya kukuza elimu hapa nchini hasa kipindi hiki Taifa linapoelekea katika
ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Kati ya hayo, 45 yamekabidhiwa kwa
wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 kwa Baraza la
Mitihani Tanzania (NECTA) .
“Imani yangu ni kuwa magari haya
yatatunzwa vizuri na yatatumika kufanya kazi na malengo yaliyokusudiwa
na si vinginevyo hivyo yatasaidia kuboresha elimu hapa nchini ”
Alisisitiza Prof. Ndalichako
Akifafanua, Prof. Ndalichako
amesema kuwa magari hayo yanalenga kusaidia Taifa kuzalisha wataalamu
wenye weledi, mahiri na wabunifu hasa katika kipindi hiki Taifa
linapoelekea katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Aliongeza kuwa Serikali haitasita
kuwachukulia hatua kali wale wote watakaotumia magari hayo kwa maslahi
binafsi na wale watakaoshindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria
na kanuni zinazosimamia sekta ya elimu.
Katika kuimarisha elimu, Prof.
Ndalichako amesema kuwa Serikali imefungua ofisi mpya 5 za udhibiti
ubora wa shule katika Halmashuri za Songwe, Kigambaoni, Ubungo, Chalinze
na Ushetu kwa lengo la kuimarisha shughuli za udhibiti ubora katika
Halmashuri.
Jambo jingine ni kuandaliwa kwa
mkakati wa Taifa wa Elimu jumuishi (2018-2021) ili kushughulikia masuala
ya elimu kwa watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalum na kutoa fursa
kwa wadau wengine wa maendeleo kupata maeneo ya kuchangia utekelezaji
wa elimu jumuishi.
Hivi karibuni Serikali kupitia
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilikabidhi pikipiki 2,894 ambazo
zimesambazwa katika halmashuri 156 katika mikoa 25, pikipiki hizo
zitasaidia waratibu elimu kata katika kutekeleza majukumu yao ili
kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa shuleni katika maeneo yao.
Magari 45 yaliyotolewa kwa
Wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya kanda na wilaya na 2 kwa Baraza la
Mitihani Tanzania (NECTA) ni chachu katika kuimarisha sekta ya elimu
hapa nchini na kuongeza ari kwa watendaji katika sekta ya elimu.
No comments:
Post a Comment