Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao kuzungumzia
azma ya Serikali ya kuboresha mfumo wa huduma za vibali vya ajira na
ukaazi nchini hii leo Juni 28, 2018 Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk. Mwigulu Nchemba akitoa ufafanuzi wa masuala ya vibali vya ajira na
ukaazi kwa waandishi wa habari walipokutana mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Uratibu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama (hayupo pichani) walipokutana Bungeni Dodoma Juni 28, 2018
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Uratibu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama (hayupo pichani) walipokutana Bungeni Dodoma Juni 28, 2018
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
………………………
NA MWANDISHI WETU
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Idara ya Uhamiaji) imekusudia kufanya
mabadiliko ya kimfumo ambayo yatahusisha utoaji wa vibali ya ajira
nchini pamoja na vibali vya ukaazi ili kuhama kutoka mfumo wa zamani na
kuwa na mfumo wa kielektroniki.
Maboresho hayo yanakwenda sambamba
na matumizi ya TEHAMA, ambapo kutakuwa na utaratibu wa kuwa na kadi
moja (smart card), ambayo itakuwa na taarifa za muhusika kuhusu kibali
cha ajira pamoja na hati ya ukaazi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alikukutana na
waandishi wa habari hii leo Mjini Dodoma (Juni 28, 2018).
Waziri Mhagama alieleza kuwa,
kuanzishwa kwa mfumo huo utasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa za
wageni nchini zenye uhakika na zitakazo patikana kwa wakati ili
kudhibiti mianya yote rushwa kwa watendaji kwa kuwa taarifa zote
zitapatikana katika kanzidata maalum.
“Uwepo na mfumo huu mpya utasaidia
kuondokana na mianya yote ya rushwa kwa Watendaji wa Serikali pamoja na
kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wageni na malengo ya ujio wao
hapa nchini kwani taarifa zote zitapatikana kwenye kanzidata
maalum,”alisisitiza Mhagama
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba alieleza kuwa mfumo huu wa kadi moja
utasaidia hutatua changamoto ya uchuleweshaji wa vibali ili kuondokana
na usumbufu wa ufuatiliji wa vibali hivyo kwa wageni.
“Lengo kubwa la mabadiliko haya ni
kuwa na kadi moja itakayomruhusu mgeni kufanya kazi kulingana na sheria
na taratibu zilizopo na kuwaondolea usumbufu usio wa lazima na kuongeza
ufanisi kwa watendaji wa Serikali,” alisisitiza Mwigulu
Aidha alitoa rai kwa Taasisi zote
zinazotumia wageni kuhakikisha wanafanya uhakiki wa taarifa za wageni
hao hususan uhalali wa kuwepo kwao pamoja na kazi wanazozifanya ili
kuepuka udanganyifu unaoweza kujitokeza.
“Nitoe rai kwa Taasisi zote
zinazotumia wageni katika ofisi zao kuhakiki na kujiridhisha taarifa za
vibali vya ajira na ukaazi wa wageni hao ili kuepuka taarifa zisizo
sahihi na kuhakikisha kila kila mgeni anakuwa na kibali halali
kinachomruhusu kuwepo nchini,”alisisitiza Mwiguli
No comments:
Post a Comment