Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akizungumza na
Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu za watalii
nchini kwa mwaka 2017 inayoonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2
milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa mwaka 2017. Kulia ni Kamishina wa
Idara ya Uhamiaji, Hannelore Manyanga na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara
ya Takwimu ya Taifa (NBS) Dkt. Albina Chuwa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsius Mdamu akizungumza na
Waandishi wa habari kuhusiana na kukua kwa kasi kwa utalii wa fukwe na
jinsi Idara ilivyojipanga kuimarisha fukwe zilizopo nchini wakati wa
uzinduzi wa taarifa ya takwimu za watalii nchini kwa mwaka 2017,
inayoonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi
kufikia 1.3 kwa 2017.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Utalii, Paskas Mwiru (katika) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya
kutathimini twakimu za watalii wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu
ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka 2017, uliofanyika leo jijini Dar
es Salam
Baadhi ya wadau wa sekta ya
Utalii wakiwa kwenye kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam cha
uzinduzi wa taarifa ya takwimu ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka
2017 huku ikionesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016
hadi kufikia 1.3 kwa 2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii, Deograsius Mdamu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na wadau wa
sekta ya utalii wakifuatilia uzinduzi wa taarifa ya takwimu ya watalii
waliokuja nchini kwa mwaka 2017,Taarifa hiyo inaonesha watalii
wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa 2017.
Picha na Lusungu Helela- MNRT
…………………
NA LUSUNGU HELELA-DSM
Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii imetaja idadi ya watalii walioingia nchini kuwa
imeongezeka kutoka Milioni 1.2 Mwaka 2016 hadi kufikia watalii Milioni
1.3 mwaka 2017 huku watalii kutoka nchini Marekani wakiwa vinara.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni kukua
kwa kasi ya uchumi huku ikisaidiwa na ujenzi wa miundombinu ya
barabara katika hifadhi za Taifa.
Mbali na idadi hiyo, Serikali
imetaja mapato yaliyopatikana kutokana na watalii hao kuwa
yameongezeka kutoka wastani wa Dola za Kimarekani Milioni 2.1 Mwaka 2016
hadi kufikia Dola Milioni 2.2 Mwaka 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen.
Gaudance Milanzi amesema taarifa ya utafiti huo unaonesha kuwa Tanzania
inazidi kufanya vizuri katika sekta ya utalii kwa vile kila mwaka idadi
ya watalii na mapato yamekuwa yakiongezeka.
Awali, Milanzi alisema ripoti
hiyo ya pamoja iliandaliwa kwa ushirikiano wa Benki Kuu Tanzania(BOT),
Tume ya Taifa ya Takwimu(NBS), Idara ya Uhamiaji Zanzibar,
Kwa mujibu wa Milanzi, ripoti hiyo
iliyopatikana kutokana na ‘survey’ iliyofanywa katika njia kuu za
watalii, ikiwemo viwanja vya ndege pamoja na maeneo ya njia za mipaka ya
kuingia nchini, pia imebaini idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini
wanatoka katika nchi za Marekani, Uingereza, India, Uholanzi pamoja na
Uswiswi.
Katika uzinduzi wa taarifa hiyo
Milanzi amesema taarifa hizo zilikusanywa kupitia viwanja vya ndege
vya Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro(KIA), Abeid Aman
Karume(Zanzibar) pamoja na mipaka ya Namanga, Tunduma, Mtukula na
kwingineko, kwa kiasi kikubwa imechangiwa na idadi ya watalii
walioingia nchini na kutembelea fukwe pamoja wanyamapori
Alisema kimsingi ongezeko la
watalii waliongia nchini, pia limetokana na kasi ya kuvitangaza vivutio
mbalimbali vilivyopo nchini inayofanywa na Bodi ya Utalii
Tanzania(TTB) kupitia mamlaka iliyopewa ya kuvitangaza vivutio hivyo,
zikiwemo mbuga za wanyama, fukwe, mlima Kilimanjaro na vinginevyo.
Aidha alisema mbali na vivutio
hivyo pia siku za hivi karibuni Tanzania imekuwa ikipata wageni
wanaofika nchini kwa ajili ya kupata matibabu katika hospitali zetu
mbalimbali, ambao pamoja na huitaji wao katika masuala ya tiba, wanapata
fursa ya kufanya utalii na hivyo kuchangia ongezeko katika eneo hilo.
Alisema ujenzi wa miundombinu ya
barabara katika Hifadhi za Taifa pia kwa kiasi kikubwa kumechangia
kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini, hatua aliyosema kuwa
itazidi kuutangaza utalii wetu.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Utalii
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Deograsius Mdamu amesema kwa sasa
idara imeanza kuwekeza nguvu katika utalii wa fukwe kwa vile ni aina ya
utalii ambao unaonekana kupendwa na watalii wengi wanaongiana nchini.
Wakati huo huo , amesema
wanataraji kushirikiana na mamlaka mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya
Uendelezaji Uchumi(EPZA) katika kutangaza utalii.
Aidha alitaja changamoto
mbalimbali zilizokuwa zinazowakabili watalii, ikiwemo masuala ya viza
pamoja na huduma za kifedha kupitia utaratibu kadi maalumu, ni maoneo
yanayoendelea kufanyiwa kazi na Wizara hiyo ili kuzidi kuutangaza utali
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment