Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Leodgar Tenga,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo mchana
wakati akitangaza rasmi \tarehe ya kutoa Tuzo za Rais za Viwanda
zinazotarajia kufanyika Mei 4 mwaka katika Hoteli ya Serena, ambapo
mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa CTI, Dkt. Samuel
Nyantahe na Makamu wa pili wa Mwenyekiti CTI, Shabbir Zavery. Picha na
Muhidin Sufiani (MAFOTO)
***************************************
Na Leandra Gabriel, Mafoto Blog, Dar
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika tuzo za Rais za Mzalishaji bora wa Viwandani
(PMAYA) za mwaka 2017 zinazotarajiwa kufanyika Mei 4 mwaka huu, jijini
Dar es Salaam.
Shindano
hilo la PMAYA zinazoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI)
hutoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri katika mwaka uliopita
likiwahusisha wanachama wa CTI na wasio wanachama.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam,mchana huu, Mkurugenzi
mtendaji wa CIT Leodger Tenga amesema kuwa tarehe 7 Desemba mwaka jana
walizindua shindano la mzalishaji bora wa kampuni na tayari kampuni 36
ziliweza kujitokeza kwenye mchakato huo ukiwa umeenda vizuri na washindi
wamepatikana ambao watakabidhiwa zawadi zao siku hiyo ya ijumaa, Mei 4.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Machapisho wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI,
Thomas Kimbunga, akitangaza utaratibu wa upatikanaji wa washiriki wa
tuzo hizo,wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, ambao ni sehemu ya waratibu mkutano huo, Teddy Mapunda, akiongoza mkutano huo,
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Machapisho wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI,
Thomas Kimbunga, akitangaza utaratibu wa upatikanaji wa washiriki wa
tuzo hizo,wakati wa mkutano huo. kutoka (kushoto) ni Meneja Masoko wa
Kampuni ya Alaf Tanzania, Theresia Mmary, Makamu wa pili wa Mwenyekiti
wa CTI, Shabbir Zavery, Mwenyekiti wa CTI, Dkt. Samuel Nyantahe na
Mkurugenzi Mtendaji, Leodgar Tenga.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Dkt. Samuel Nyantahe, akizungumza na waandhishi wa habari kuhusu tuzo hizo.
********************************************
Kwa
upande wa mwenyekiti wa shirikisho hilo Dkt. Samwel Nyantahe ameeleza
kuwa shirikisho hilo ni la wamiliki wa viwanda nchini ni kwa lengo la
kuweka mazingira ya uzalishaji nchini na shindano hilo linatoa nafasi ya
kutangaza bidhaa kwa wafanyabiashara na kupata nafasi ya kukutana na
Rais na kuzungumza naye ikiwa ni muhimu kwa kuwa tunaelekea katika
uchumi wa viwanda.
Mashindano
hayo yanahusisha zaidi ya sekta 18 na makampuni 36 na kuna zawadi
maalumu kwa washindi wa matumizi bora ya nishati katika viwanda vyao.
Mkurugenzi
wa machapisho wa (CTI) Thomas Kimbunga ameeleza kuwa namna ya kushiriki
ilikuwa katika makundi matatu ya viwanda yaani vile vikubwa, vidogo na
vya kati na washiriki wameshindanishwa kulingana na makundi
waliyoshindania na vigezo katika kila kundi ni pamoja na mazingira,
mahusiano kazini na kuendeleza wafanyakazi sambamba na suala la ubora wa
bidhaa kwa kuthibitishwa na TBS.
Aidha
ameeleza kuwa shindano hilo litatasaidia kuongeza ufanisi hasa katika
utendaji kazi katika sekta mbalimbali za viwanda pia washiriki watapata
nafasi ya kujua maeneo waliyofanya vizuri na kupata nafasi ya kuboresha
vyema bidhaa zao.
Baadhi
ya vigezo ambavyo vimezingatiwa ni pamoja na faida kwa jamii, afya na
usalama, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, utendaji kiuchumi, utendaji
kiteknolojia na matumizi bora ya nishati.
Sehemu ya wanahabari wakiwa bize kurekodi hotuba ya Mwenyekiti huyo.
Wanahabari wakiwa kazini…..
Baadhi ya wageni waalikwa katika mkutano huo….
Mwakilishi wa Hoteli ya Serena ambao ni moja kati ya wadhamini, Meneja wa mikutano na matukio, Alex Maboko, akizungumza jambo.
No comments:
Post a Comment