Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na
wadau wa kutoka Shirika la ‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea
Kusini wakati walipofika katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma
kuwasilisha Mpango maalum kuhusu Umuhimu wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra
na Mitazamo katika Kujiletea Maendeleo .
Katibu Mkuu Shirika la
‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini Dkt. Hun Mok Lee
(kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo hapa Tanzania Jeon Hee Young
wakitoa mafunzo kwa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kuhusu
uzingatiaji wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra na Mitazamo katika Kujiletea
Maendeleo Jumuishi.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti
ya Idara kuu Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mafunzo maaalum kuhusu
uzingatiaji wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra na Mitazamo katika Kujiletea
Maendeleo yaliyowasilishwa na ujumbe kutoka Shirika la ‘International
Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini katika ukumbi wa Wizara jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu Bw. Raphael Nombo akichangia jambo wakati wa kikao kati
ya Wizara na wadauwa Maendeleo kutoka Shirika la International Youth
Fellowship kutoka Korea Kusini katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii
Bw.Patrick Golwike akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Wizara na
wadau wa Maendeleo kutoka Shirika la ‘International Youth Fellowship’
kutoka Korea Kusini katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto
Bi. Magreth Mussai akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Wizara na
wadau wa Maendeleo kutoka Shirika la ‘International Youth Fellowship’
kutoka Korea Kusini katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga na Menejimenti yake
wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa maendeleo wa Shirika la
‘International Youth Fellowship’ kutoka Korea Kusini mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha kujadili uzingatiaji wa Elimu ya Mabadiliko ya
Fikra na Mitazamo katika kujiletea Maendeleo Jumuishi kilichofanyika
katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akifurahia jambo na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la International Youth Fellowship kutoka
Korea Kusini Bw. Jeon Hee Young mara baada ya kumalizika kwa kikao
kilichojadili uzingatiaji wa Elimu ya Mabadiliko ya Fikra na Mitazamo
katika Kujiletea Maendeleo .
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………..
Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inategemea kunufaika na mradi maalum kutoka Shirika la
‘International Youth Fellowship’ lenye makazi yake nchini Korea ya
Kusini
kuhusu utoaji wa mafunzo ya kuiwezesha jamii kuwa na tabia, fikra
na mtazamo chanya ili kuwa na ari na hamasa ya kufikia mabadiliko ya
kweli na endelevu katika kujiletea maendeleo ya jamii yenyewe na Taifa
kwa ujumla.
Akizungumza katika Kikao kati ya
Serikali na Shirika hilo Katibu Mkuu Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa Mradi huu ni
muhimu sana katika jamii ya watanzania kwani utasaidia kubadilisha fikra
za watanzania katika kukuza ari na raghba ya kujiletea maendeleo
wenyewe katika maeneno yao.
Bibi Sihaba ameongeza kuwa elimu
hii itasaidia kuimarisha fikra chanya kwa watanzania wote kujitambua na
kuona kuwa maendeleo ya kweli na endelevu yanatokana na ufahamu, uelewa
na utashi wa wananachi waliojitoa kufanya kazi za maendeleo kwa
kushirikiana na Serikali yenyewe ili kutatua changamoto zilizopo na
hivyo kujifikia maendeleo jumuishi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa
ujumla.
Aidha, akizungumza wakati akitoa
elimu hiyo kwa ujumbe wa Menejimenti ya Idara kuu Maendeleo ya Jamii,
Katibu Mkuu wa Shirika la ‘International Youth Fellowship’ Dkt. Hun Mok
Lee amesema kuwa mabadiliko ya fikra ni muhimu katika mendeleo ya Taifa
lolote na kama Tanzania inataka kuendelea zaidi inabidi ianze kutoa
elimu itakayosaidia kuwajenga na kubadili fikra za watoto na vijana
kuhusu utashi wao wa kutatua vikwazo na changamoto ili kujiletea
maendeleo yao wenyewe.
Dkt. Lee ameongeza kuwa ili kuwa
na taifa imara zaidi Serikali haina budi kuwarithisha wananchi elimu
itakayowawezesha kuwa tayari wa kubadili mtindo wa maisha yao kwa kuwa
na mtazamo mmoja wa kushirikiana pamoja katika kila jambo ili kuchangia
azma ya kufikia maendeleo thabiti ya watu na Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kuwa Mradi huu unaendana
kabisa na dhana ya maendeleo ya jamii na utasaidia kuongeza chachu
katika kuleta mabadiliko ya fikra za wananchi kuweza kujitoa kwa dhati
kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha kuwa maisha ya
watanzania yanashamiri na uchumi wa Taifa unapaa.
Katika kutekeleza mpango huu,
Wataalam wa Maendeleo ya jamii wataendelea kuraghibisha jamii kubadili
tabia zao kutoka katika desturi za uchumi wa vijungu jiko na imani hasi
na hivyo kuwa na fikra chanya zinazochochea azma ya kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment