MJUMBE wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Mjini na viongozi mbali mbali
wa Chama mara baada ya kupokea taarifa ya hali ya kisiasa ya Mkoa wa
mjini, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk.Abdulla Juma Mabodi(Katikati), Mkuu
wa Mkoa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud(kushoto).
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia ngoma ya
asili na kuwatuza wasanii wa ngoma hiyo mara baada ya kuweka jiwe la
msingi katika Ofisi ya UWT iliyopo Aman Mkoa wa Mjini.
NAIBU Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akizungumza na wananchi wa
jimbo la Kikwajuni katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa
maji safi na salama unaosimamiwa na Mbunge na Mwakilishi wa jimbo hilo,
mradi huo umewekwa jiwe la msingi leo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan.
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wana CCM
wa Jimbo la Jang’ombe mara baada ya kutembelea jengo jipya la Tawi la
CCM Jang’ombe Urusi .
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka Jiwe la msingi
katika mradi wa maji safi na salama Jimbo la Kikwajuni Unguja.
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Chuo cha
Mwenge Community Centre kinachotoa Mafunzo ya ufundi na Amali yakiwemo
Ushoni, Computer, Uandishi wa Habari, Umeme na Uuguzi, kinachomilikiwa
na CCM Mkoa wa Mjini.
MBUNGE wa Jimbo
la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni (wa kwanza kulia anayezungumza)
akiwatambulisha madiwani wawili wa jimbo hilo kwa Mhe. Samia Saluhu
Hassan katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika tanki la maji
safi na salama lenye uwezo wa kuchukua lita zaidi ya 200,000.
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mchoro wa
mfumo wa usambazaji maji katika Jimbo la Kikwajuni.
MWENYEKITI wa
jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Jimbo la Shauri Moyo, Makame Kai
akizungumza mbele ya mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM taifa Mhe.
Samia Suluhu Hassan katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Ofisi
ya Jumuiya hiyo iliyopo mtaa wa Mkele Trade Skuli.
MWENYEKITI wa
jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Jimbo la Shauri Moyo, Makame Kai
akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM taifa Mhe. Samia
Suluhu Hassan katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Ofisi ya
Jumuiya hiyo iliyopo mtaa wa Mkele Trade Skuli.
………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU wa Pili wa Rais,Samia
Suluhu Hassan, amewataka wananchi wa visiwa vya Zanzibar kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na Wabunge na Wawakilishi wa majimbo ili
waongeze
ari na kasi ya utatuzi wa kero zinazoikabili jamii.
Rai hiyo ameitoa leo katika
mwendelezo wa ziara yake visiwani Zanzibar alipokutana na wanachama wa
CCM na wananchi wa jimbo la Kikwajuni na kuzungumza nao katika hafla
ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa tanki la maji
safi na salama lenye uwezo wa kuhifadhi lita zaidi ya 200,000 katika
jimbo la kikwajuni.
Amesema endapo wananchi watakuwa
mstari wa mbele kuthamini miradi ya wabunge na wawakilishi kwani
inatekelezwa kwa lengo la kumaliza changamoto zinazoikabili jamii.
“Wananchi mkiwa na umoja na
kushirikiana kulinda na kuthamini yale yote mazuri yanayofanywa na
viongozi wenu basi itakuwa rahisi sana kutatua kero zenu kwa wakati”,
amesema Mhe. Samia
Pia amewataka wabunge na
wawakilishi wa majimbo mbali mbali kuwa na maelewano mazuri mazuri kwa
lengo la kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi.
Amesema kitendo cha viongozi hao
kutokuwa na maelewano mazuri yanasababisha kukwamisha na
kuwacheleweshea wananchi kupata maendeleo kwa wakati.
Makamu huyo wa Rais ameongeza kuwa
kuna baadhi ya majimbo ambayo viongozi hao hawana ushirikiano na kwamba
wanafikia hatua hawaongeii na kutofikiria kuleta maendeleo.
“Kuna majimbo ambayo wananchi wao
wanakumbwa changamoto ya ukosefu wa maji na elimu na kwamba unakuta
viongozi hao kati ya Mbunge na Mwakilishi hawafikirii kutatua kero za
wananchi hizo kutokana na kuwa hawana ushirikiano,”amesema Samia.
Mbali na hilo katika ziara hiyo
Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa tanki la
maji safi na salama jimbo la Kikwajuni pamoja na jiwe la msingi la ofisi
ya tawi la Chama Cha Mapinduzi(CCM) Jang’ombe Urusi.
Hata hivyo aliwataka wananchi wa
jimbo la Kikwajuni kuhakikisha wanatunza miradi ya maendeleo ya maji na
kwamba wanatakiwa kuanzisha kamati ya jimbo kwa lengo la kusimamia
miradi hiyo ili iwe endelevu.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Mabodi, amesema CCM ipo kikazi na inaenda na
wakati katika kutatua kero za wananchi.
Ameeleza kuwa CCM inawahakikishia
wananchi kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imejipanga
kuwatatulia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji ambapo
inaendelea kutekeleza miradi ya maji ili kuhakikisha mikoa yote ya
Zanzibar inapata huduma hizo.
Naibu huyo ameeleza katika kipindi
hichi cha dharura SMZ na kushirikiana mradi wa Ras Al Khaimah imechimba
visima 120 vya maji visiwani Zanzibar.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,
Hamad Yussuf Masauni, amesema kupitia mradi huo wa maji wa awamu ya
pili utatatua changamoto ya upatikanaji wa maji unatokana na miundombinu
ilioko zamani ambapo nyingi zilikuwa mibovu mengine ilipasuka na
kuziba.
“Baada ya kumalizika mradi huu
tunafumua mfumo wa maji wa jimbo la kikwajuni na tunaweka mfumo mpya wa
kwetu ambao safari hii maji yatapatikana kwa urahisi na wananchi
mtafurahi,”amesema Mhe. Samia.
Aidha ametembelea ujenzi wa Tawi
la CCM Jang’ombe Urusi na kuwapongeza viongozi wa Jimbo la Jang’ombe kwa
utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM na kuwataka wawe walimu wa majimbo
mengine.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia ameweka Jiwe la msingi katika
Ofisi ya Watu Wenye Ulemavu Jimbo la Shauri Moyo Unguja, na kuipongeza
jumuiya hiyo kwa ubunifu wao wa kujenga ofisi ya kuzalisha kipato.
Amezitaka familia zenye watu wenye
ulemavu kuwapeleka katika ofisi hiyo ili wajifunze fani mbali mbali
zitakazowasaidia katika maisha ya kila siku.
Ameahidi kutatua hatua kwa hatua
changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo ambazo ni pamoja na ukosefu wa
viti vya watu wenye ulemavu, mashine ya photokopi ya rangi na mahitaji
mengine.
Katika Hafla hiyo Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Mabodi amesema Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar imeahidi kuchangia shilingi 500,000 kwa ajili ya kuunga
mkono juhudi za watu wenye ulemavu.
Hata hivyo ametembelea Chuo Cha
Mwenge Community Centre kinachotoa mafunzo ya fani mbali mbali yakiwemo
ya ushoni, umeme, computer, Uuguzi na Uandishi wa habari
kinachomilikiwa na CCM Mkoa wa mjini.
Mapema Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini
Ndugu Mohamed Nyawenga alisoma na kumkabidhi taarifa ya hali ya kisiasa
kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Bi. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia kikao hicho aliwataka
viongozi na watendaji wa Mkoa huo kufanya kazi kwa bidii sambamba na
kulinda heshima ya Mkoa huo wenye historia kubwa ya uimara wa kisiasa na
kijamii nchini.
Pia amewaagiza kutunza vizuri miradi ya maendeleo inayomilikiwa na Mkoa huo ili kwenda sambamba na sera ya siasa na uchumi.
No comments:
Post a Comment