Washindi wa wiki ya nne katika picha ya pamoja
Washindi wa pikipiki wakifurahi baada ya kukabidhiwazawadi zao.
Washindi wa pikipiki wakifurahi baada ya kukabidhiwazawadi zao.
Baadhi ya washindi wakisubiri kupokea zawadi katika hafla hiyo.
Wakati promosheni ya mzuka wa Soka
na Coka imeingia katika wiki ya 4 tangu izinduliwe ,zaidi ya wakazi 32
wa mikoa ya, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida wamejishindia
zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa za pikipiki,Luninga bapa za
kisasa na fedha
taslimu shilingi 100,000/-
Akiongea katika hafla ya kukabidhi
zawadi kubwa kwa washindi wa wiki ya nne,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa
Bonite Bottlers, Chris Loiruk,alisema
kumekuwa na ongezeko la washindi
katika wiki ya nne tangu kuanza kwa promosheni hiyo,na kampuni inayo
furaha kuona wateja wake wanaendelea kushiriki katika promosheni hii na
kuweza kujishindia zawadi mbalimbali.
“Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa
kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha
taslimu kuanzia 5,000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito
waendelee kushiriki waweze kujishindia”,Alisema Loiruk.
Washindi wapatao 18 ambao
walikabidhiwa zawadi zao za Pikipiki,Luninga na Fedha taslimu katika
hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite mwishoni mwa wiki
waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo
wa kuwakwamua wateja wake kiuchumi.
Akiongea kwa niaba ya washindi
waliokabidhiwa luninga, Denis Stanslaus mkazi wa Rau Madukani, Manispaa
ya Moshi,alisema wamefurahi kupata zawadi za luninga za kisasa hususani
katika kipindi hiki kuelekea mashindano ya kombe la dunia kwa kuwa
wataburudika na mashindano hayo na familia zao na kupata habari kupitia
luninga bapa za kisasa.
Akiongea kwa niaba ya washindi wa
pikipiki, Jackline Emmanuel, mkazi wa Kijenge Juu Mkoa wa Arusha
,alisema kuwa wanayo furaha kubwa kwa zawadi waliyojishindia na chombo
hicho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha usafiri sambamba na
matumizi ya biashara kwa ajili ya kuongeza pato la familia.
Kwa upande wake, Elinaisha Nasari ,
Mkazi wa Tengeru Mkoa wa Arusha , akiongea kwa niaba ya washindi wa
fedha taslimu shilingi 100,000/-alisema kuwa fedha walizojishindia
zitawawezesha kutatua matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiwakabili
sambamba na kuongeza mitaji yao ya biashara.
No comments:
Post a Comment