Mkuu wa Mkoa wa Pwani
,Mhandisi Evarist Ndikilo ,akipanda mche mpya wa zao la mkorosho
,wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miche mipya ya mikorosho Mkoani hapo
,uliofanyika ,Ruvu Jkt,huko Vikuruti Kibaha Vijijini.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj
Majid Mwanga ,akipanda mche mpya wa zao la mkorosho ,wakati wa uzinduzi
wa upandaji wa miche mipya ya mikorosho Mkoani hapo ,uliofanyika ,Ruvu
Jkt,huko Vikuruti Kibaha Vijijini.
Picha na Mwamvua Mwinyi
…………….
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi
Evarist Ndikilo, amewahimiza wawekezaji wenye uwezo wa kujenga viwanda
vya kubangua korosho na kutengeneza magunia ,kujenga viwanda hivyo
ili
kuwarahisishia wakulima wa zao hilo .
Aidha amewaasa maafisa ugani
mkoani hapo, kuacha kujibweteka maofisini kupigwa viyoyozi na badala
yake watoke na kwenda kwa wakulima kutoa elimu mbalimbali za kilimo cha
kisasa na chenye tija cha zao hilo.
Alkadhalika, Ndikilo amewataka
wakulima wa zao la korosho kufufua mashamba ya korosho pamoja na kupanda
miche mipya ya mikorosho ili kuinua zao hilo kimkoa.
Akizindua upandaji wa miche mipya
ya mikorosho Ruvu JKT ,Vikuruti wilayani Kibaha Vijiji, alieleza msimu
uliopita ulikumbwa na changamoto ya upungufu wa magunia hivyo kuna kila
sababu ya kujengwa viwanda hivyo ili mkulima aweze kuwa na uhakika wa
kupata magunia.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, miaka
ya 60/70 mkoa wa Pwani ulikuwa ukizalisha kwa wingi lakini kwasasa
mashamba mengi yametelekezwa hivyo kusababisha kushuka kwa kilimo hicho .
“Baadhi ya wakulima walishindwa
kupalilia,kuweka dawa na mashamba mengi yalitelekezwa, kutokana na hilo
nachukua fursa hii kutoa rai kwa maafisa ugani, mtoke maofisini,
mkawaelimishe wakulima wetu kuhusiana na kilimo chenye tija,na
muwahimize wapande miche mipya”
“Tumeamua kufanya uzinduzi huu ili
kuonyesha umuhimu wa zao hili kimkoa na kitaifa kama mjuavyo serikali
yetu ya awamu ya tano imeliingiza zao hili kuwa moja ya mazao ya
kimkakati ikiwemo pamba, kahawa ,tumbaku na chai”, Katika kipindi hiki
cha kujenga uchumi wa kati na viwanda ili kuinua pato la Taifa
“alifafanua Ndikilo.
Hata hivyo ,Ndikilo aliwataka
viongozi wa vitongoji na vijiji kuanzisha madaftari ya wakulima kwa
lengo la kupata takwimu zao na kuwafuatilia katika mipango mbalimbali ya
masuala ya kilimo.
Awali afisa kilimo wa mkoa wa
Pwani, Specioza Kashangaki alieleza , kutokana na umuhimu wa zao la
korosho, serikali kupitia bodi ya korosho Tanzania imesambaza mbegu bora
ili miche itakayopatikana isambazwe bure kwa wakulima.
Alisema kupitia utaratibu huo mkoa
huo ulipokea kilo 7,182 zinazokadiriwa kutoa miche milioni.1.039,687
ambazo inatarajiwa kupandwa kote mkoani kipindi cha mvua za masika.
Specioza alitaja changamoto
zinazowakabili kuwa ni kutokuwepo na kumbukumbu sahihi za miche mipya
inayopandwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa na kutokuwepo kwa maghala
bora ya kuhifadhia korosho hali inayoathiri ubora wa korosho.
“Anabainisha”Kumekuwepo na
udanganyifu mkubwa unaofanyika katika maghala ya kuhifadhia korosho
ambapo baadhi ya AMCOS zimebainika kusabababisha uzito wakati wa mazao
kutofautiana na uzito wa korosho wakati mnunuzi anakabidhiwa korosho
zake.
Akitoa taarifa ya uendelezaji wa
zao hilo,katika shamba la Ruvu JKT ,meneja wa shamba , Godfrey Mwakabole
alisema kitaalamu mikorosho inatakiwa kupandwa kwa nafasi mita 12 kwa
mita 12, na kupata miche 28-30 kwa hekari moja.
Kwa mujibu wa Mwakabole alisema,
wamepanda miche mipya katika hekari 50 ambapo wamechanganya na zao la
mahindi na shamba jingine la hekari 50 wamepanda miche hiyo na
wanakaribia kuanza palizi.
Miche ya mikorosho inatakiwa
kutunzwa kwa kupaliliwa, kutengenezewa visahani, kupogolea,kudhibiti
magonjwa na wadudu ambapo inashauriwa mikorosho ikiwa midogo kuchanganya
mazao ya muda mfupi ili wakulima wapate mazao na kipato kwenye eneo
moja.
No comments:
Post a Comment