
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mkinga,Mhandisi Michael Ndunguru (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza
wadau mbalimbali kufungua bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa
Mkinga mkoani Tanga.
Wadau wa mradi wa maji wa Mkinga wakibeba ndoo kwa pamoja wa hafla ya uzinduzi wa mradi.
Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa
Shirika la Water Missions International Tanzania, Isack Abdiel,
akielezea mradi huo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo.
Kisima cha maji kilichokuwa kinatumika kabla ya mradi mpya.
Sehemu ya miuondombinu ya mradi mpya.
Shirika la Kimataifa
linalojishughulisha na kusambaza huduma za maji la Water Missions
International Tanzania, mwishoni mwa wiki limezindua mradi mkubwa
utakaonufaisha vijiji 7 vya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utaowawezesha
wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa matumizi yao
na matumizi mengineyo na shughuli za kiuchumi.
Kwa kipindi cha muda mrefu wilaya
ya Mkinga imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa maji salama,
kutokana na kutokuwepo na vyanzo vya uhakika vya maji katika eneo
hilo.Vijiji 4 vya Mkinga, Mtenguleni, Mwakihonda and Karoyo vimekuwa
vikitegemea kupata maji ya bomba kutoka tanki la zamani la kusambaza
maji kutoka kijji jirani cha Parangukasere, ambalo limekuwa
halitoshelezi mahitaji ya maji kwa wakazi wa vijiji hivyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mkinga,Mhandisi Michael Gregory Ndunguru,ambaye alikuwa mgeni rasmi
wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa
Mkinga,kuzinduliwa kwa maradi huu wilayani hapa kutawezesha wananchi
kupata maji safi ya uhakika wakati wote,kwa niaba ya serikali
nalishukuru shirika la Water Missions International Tanzania kwa kuunga
mkono jitihada za serikali ya Tanzania ya kukabiliana na changamoto za
uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini”.
Mhandisi Ndunguru, alisema mradi
huu utanufaisha maisha ya mamia ya wananchi wakazi wa Mkinga na
kupunguza adha kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi
kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kifamilia . Alitoa wito kwa
wakazi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa shirika hilo sambamba na
kutunza miundo mbinu itakayowekwa katika maeneo yao ili kuwezesha mradi
kuwa endelevu.
“Mradi huu muhimu hapa Mkinga pia
utaimarisha afya na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa mbalimbali
yanayosababisha na ukosefu wa maji na matumizi ya maji yasiyo salama kwa
kuwa hivi sasa tuna uhakika wa kupata maji salama,”alisisitiza.
Kwa upande wake,Mratibu wa Huduma
za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania ,Isack
Abdiel alisema “Tunayo furaha kuzindua mradi wa maji katika wilaya ya
Mkinga ,ukiwa ni mwendelezo wetu wa kuunga mkono serikali ya Tanzania
kuboresha upatikanaji wa maji ya uhakika na salama kwenye jamii zenye
upungufu wa maji nchini,tunayo imani wananchi mmeupokea vizuri na
mtaulinda ili uwe mradi endelevu ili unufaishe mpaka vizazi vijavyo”.
Aliwashukuru watendaji wa
serikali,mashirika yasiyo ya kiserikali inayoshirikiana nayo na wadau
wote ambao wamefanikisha jitihada za kuanzisha mradi huu wilayani
Mkinga.
Shirika la Water Missions
International Tanzania,lilianza kufanya kazi nchini mnamo mwaka 2013,
likiwa limejikita katika kuendesha miradi ya kuondoa kero ya maji kwenye
jamii ,sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu miradi ya
maji.Hadi kufikia sasa shirika limefanikisha miradi ya maji katika mikoa
zaidi ya 6 nchini,ikiwemo mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Kagera na
Tanga.
Ofisi za makao makuu ya Water
Missions International Tanzania nchini yapo jijini Dar es alaam na ndipo
inaporatibiwa miradi yote ya maji inayoendeshwa na shirika nchini
.Tanzania ni nchi ya 10 kuwa na miradi ya shirika hili.Baadhi ya nchi
nyingine linapoendesha miradi ya maji ni Kenya, Uganda, Malawi, Haiti,
Honduras, Mexico, Peru, na Belize.





No comments:
Post a Comment