Jaji Mfawishi wa Mahakama
Kuu-Kanda ya Mtwara, Mhe. Jaji Fauz Twaib (kushoto) akifurahia jambo na
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Paul
Kihwelo.
Baadhi ya Waheshimiwa Majaji wa
Mahakama Kuu wanaoshiriki katika Mafunzo wakiwa katika kazi ya kikundi
‘group work’, Mafunzo hayo yanafanyika AICC mkoani Arusha.
Majadiliano yakiendelea.
Waheshimiwa Majaji wakiendelea kujadiliana.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama
………………..
Na Mary Gwera
Mahakama
Jumla ya Majaji 32 wa Mahakama Kuu
ya Tanzania wanaendelea kupatiwa Mafunzo jijini Arusha lengo likiwa ni
kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
Katika mahojiano maalum na Mkuu wa
Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto yaliyofanyika Machi 26, 2018
katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, Mhe. Jaji Dkt. Paul
Kihwelo amesema kuwa Majaji hao wanaoshiriki katika Mafunzo hayo ni wa
awamu ya pili.
“Mafunzo haya ya siku tano (5)
yaliyoanza Machi 24 na kumalizika Machi 28, 2018 yamejikita katika
maeneo mawili ambayo ni ‘Namna ya uendeshaji wa Mashauri ya Kikatiba’ na
‘Matumizi ya TEHAMA katika kutoa haki,” alisema Mhe. Kihwelo.
Mhe. Jaji Kihwelo alisema kwa kuwa
moja ya Vipaumbele vya Mahakama katika Mpango Mkakati wake ni pamoja na
Matumizi ya TEHAMA, hivyo wameona ni vyema kutoa mafunzo kwa awamu ka
Waheshimiwa Majaji na Watumishi wengine ili kujua matumizi ya TEHAMA na
changamoto zake.
Mkuu huyo wa Chuo amesema kuwa
mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo Waheshimiwa Majaji juu ya maeneo
hayo na vilevile kujenga taswira chanya ya Mahakama.
“Katika mafunzo haya, Waheshimiwa
Majaji wamepewa ufafanuzi juu ya Sera ya TEHAMA ya Taifa pamoja na
mifumo ili wakati wakati watumiapo Vifaa vya TEHAMA pamoja na mifumo
yake iliyopo Mahakamani wazingatie taratibu na miongozo kama
zilivyoainishwa katika Sera hiyo,” alifafanua Mhe. Jaji Kihwelo.
Mhe. Kihwelo aliendelea kusema
kuwa baada ya Mafunzo hayo kukamilika wanatarajia kuwa na uelewa wa
pamoja ili kurahisisha utekelezaji wa lengo la Mahakama ya kuwa Mahakama
mtandao ‘e-Judiciary’.
Aidha Mhe. Jaji Kihwelo aliongeza
kuwa wanatarajia Weledi wa Majaji kuongezeka juu ya namna bora zaidi ya
uendeshaji wa Mashauri ya Kikatiba.
“Mashauri ya Kikatiba ni Mashauri
ambayo hupelekwa Mahakamani kupinga ukiukwaji wa Katiba au kudai haki ya
Kikatiba,” alifafanua Mhe. Kihwelo.
Mhe. Jaji Kihwelo anafafanua zaidi
kuwa Mashauri ya Kikatiba ni mashauri ambayo hufunguliwa Masjala Kuu ya
Mahakama Kuu inapokaa kama Mahakama ya Kikatiba na huendeshwa na Majaji
watatu.
Mafunzo haya ya Waheshimiwa Majaji
yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa ufadhili wa fedha za Mradi wa
Benki ya Dunia na kuratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
No comments:
Post a Comment