Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Mhe. Antony Mavunde, na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko,
leo Jumanne Februari 27,2018 wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye mgodi
wa almasi wa El – Hilal Minerals Limited uliopo katika kijiji cha
Maganzo kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Manaibu
Waziri hao walikuwa wameambatana na maafisa kutoka WCF na Ofisi ya Kazi
,lengo la ziara hiyo ikiwa ni kubaini kama wamiliki wa mgodi huo
wanatekeleza sheria za uendeshaji.
Wakati
Mheshimiwa Mavunde alikuwa akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (Workers Compensation Fund -WCF), Mhe.
Biteko alikuwa akifuatilia kwa nini mgodi huo haujawasilisha wizarani
mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na mpango wa
uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR).
Akiwa
katika mgodi huo Mhe. Mavunde alibaini kuwa Mgodi huo bado ulikuwa
haujajisajili na Mfuko wa WCF na badala yake uongozi ulipeleka michango
siku moja kabla ya ziara ya Naibu waziri huyo kufika katika mgodi huo.
“Serikali
inataka waajiri wazingatie sheria, na ninyi mmevunja sheria kwa
kutojisajili, ingawa mmelipa michango yenu jana, ninachoweza kusema,
agizo la serikali la kuwafikisha mahakamani waajiri ambao hawajajisajili
nchi nzima liko pale pale, ni juu yenu kutekeleza hilo kabla
hamjapelekwa mahakamani”, alisema Mhe. Mavunde.
Mh.
Mavunde pia alibaini kuwa mgodi huo hautoi mikataba ya kudumu kwa
wafanyakazi,wafanyakazi kufanyishwa kazi zaidi ya muda wa kazi bila
malipo,wafanyakazi kutopewa vifaa kinga na mishahara kutolipwa kwa
wakati na kuwaagiza kurekebisha mapungufu yaliyopo kwenye mgodi huo
ndani ya siku 30.
“Nawapa
siku 14 za kujisajili WCF na kurekebisha mapungufu yaliyopo hapa ndani
ya siku 30,ni lazima tutii na kuziheshimu sheria zetu wanaokiuka sheria
tunawafikisha mahamani”,alisema Mhe. Mavunde.
Ziara ya
Naibu Waziri Mavunde ni muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 26,
2018 jijini Mwanza ambapo aliagiza kufikishwa mahakamani waajiri watatu
jijini Mwanza ambao hawajajisajili katika mfuko wa WCF.
Mhe.
Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko
haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri
anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko.
“Ni kosa
la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha
71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa
aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,
kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja,Nitoe wito
kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza
sheria”,alisema.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Mhe. Antony Mavunde akizungumza katika mgodi wa almasi wa El –
Hilal Minerals Ltd leo Februari 27,2018 akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi -WCF. Kulia ni Naibu
Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko. Kushoto ni Meneja Rasilimali Watu wa
Mgodi huo,Gofrey Leshange. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Kulia ni Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko akielezea namna mgodi huo unavyokiuka sheria na kuwataka kuwasilisha
wizarani mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na
mpango wa uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social
Responsibility-CSR).
Katikati ni Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Mhe. Antony Mavunde akiangalia mikataba ya wafanyakazi katika
mgodi huo ambapo alibaini kuwa mgodi huo hautoi mikataba ya kudumu kwa
wafanyakazi na kuwataka kurekebisha mapungufu hayo ndani ya siku 30.
Kulia ni
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF ,Laura Kunenge na Kamishna wa Kazi
Msaidizi nchini Rehema Moyo wakiangalia mikataba ya wafanyakazi katika
mgodi huo na kubaini kuwa kuna ukiukwaji wa sheria.
Wa pili kushoto ni Meneja
Rasilimali Watu wa Mgodi huo,Gofrey Leshange akijitetea kwanini hawatoi
mikataba ya kudumu kwa wafanyakazi wao na badala yake wanatoa mikataba
ya miezi sita hadi mwaka mmoja.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Mhe. Antony Mavunde akiusisitiza uongozi wa mgodi huo kuzingatia
sheria za nchi la sivyo watawafikisha makahamani.
Mazungumza yakiendelea katika mgodi huo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde na Naibu
Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko wakielekea katika eneo la uzalishaji wa
almasi katika mgodi wa El – Hilal uliopo Kishapu mkoani Shinyanga
Kushoto
ni Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi huo,Gofrey Leshange akielezea namna
uzalishaji wa almasi unavyofanyika katika mgodi huo
Mfanyakazi wa mgodi huo “Plant Manager”,Peter Mayeka akielezea jambo
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko wakitoka katika chumba cha kuhifadhi almasi katika mgodi wa El – Hilal
Mwenyekiti wa wafanyakazi katika mgodi wa almasi wa El – Hilal Evarist Seleman akielezea changamoto zilizopo katika mgodi huo.
Kushoto
ni Mhasibu katika mgodi wa El- Hilal Amour Nassor akijitetea baada ya
wafanyakazi wa mgodi huo kuwaeleza manaibu Waziri hao kuwa mgodi huwa
haulipi Overtime na mishahara kucheleweshwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde na Naibu
Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko wakisaini vitabu vya wageni katika
ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga baada ya kuwasili
mkoani Shinyanga kueleza lengo la ziara yao. Katikati ni Katibu wa CCM
mkoa wa Shinyanga, Haula Kachwamba
Naibu
Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko akizungumza katika ofisi ya Katibu
Tawala mkoa wa Shinyanga walipowasili mkoani Shinyanga kuueleza uongozi
wa mkoa lengo la ziara yao.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Mhe. Antony Mavunde akielezea zaidi kuhusu ziara yake na
mwenzake mkoani Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume akisoma taarifa ya mkoa kwa manaibu waziri hao.
Afisa Kazi Mfawidhi mkoa wa Shinyanga,Revocatus Mabula akizungumza.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Mhe. Antony Mavunde akimweleza mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,Josephine Matiro (kulia) lengo la ziara yao.
Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko akizungumza katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga (Josephine Matiro – kulia).
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment