Pages

Thursday, February 1, 2018

DOKTA MPANGO ATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA BARCLAYS KUHUSU RELI YA KISASA NA MRADI WA UMEME WA STIEGLER'S GORGE


                                                                              

Awali, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anaye hudumia kundi la benki za Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Bw. Peter Matlare, ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia kikamilifu uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.

Alisema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Kiafrika na Duniani kwa ujumla ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza uchumi jumuishi unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na vijijini.

Bw. Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka ushiriki wake katika ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali kuwa kipaumbele chake.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare akielezea umuhimu wa kushirikiana katika kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Benki yake wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakifuatilia mazungumzo kati yao na ugeni kutoka Benki ya Barklays nchini Afrika Kusini (hawako pichani), mkutano uliofanyika mjini Dodoma
Ujumbe kutoka Benki ya Barclays uliongozwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (kulia), wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati yao na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (hayupo pichani), kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano katika kukuza biashara kati ya Tanzania na benki yake, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Maafisa Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment