Pages

Monday, January 1, 2018

TANGAZO LA UHAKIKI WA WASTAAFU

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR
At three per cent, the retirees still trail inflation or the cost of living measure—which stood at 8.5 per  cent last year. FILE PHOTO | NMG                          
                             MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF) UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOPOKELEA PENSHENI ZA ZSSF KUPITIA BENKI TOFAUTI KUWA UHAKIKI KWA WANACHAMA UMEWADIA.
KWA WASTAAFU WOTE WA UNGUJA NA PEMBA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA TAREHE 02 JANUARI 2018 HADI 07/01/2018 KUANZIA SAA 2:00 ZA ASUBUHI.  
UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KATIKA OFISI ZA ZSSF KILIMANI MNARA WA MBAO NA TIBIRINZI CHAKECHAKE PEMBA.
INASISITIZWA KUWA UHAKIKI HUO NI KWA SIKU SITA TU. WASTAAFU WATAKAPOKWENDA KUHAKIKIWA WANATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA ZSSF NA ASIYEHAKIKIWA PENSHENI YAKE ITAZUIWA.
AIDHA WASTAAFU WOTE AMBAO HADI LEO HAWAJAFUNGUA AKAUNTI ZA BENKI NA KUWASILISHA NAMBARI ZAO KWA AJILI YA KUPITISHIA MALIPO YAO YA PENSHENI ZSSF, WANATAKIWA KUHARAKISHA KUFANYA HIVYO. MNAARIFIWA KUWA HAKUTAFANYIKA MALIPO YEYOTE KWA NJIA YA FEDHA TASLIM KUANZIA MWEZI HUU WA JANUARI 2018.
KILA ATAKAYESIKIA TANGAZO HILI AMUARIFU MWENZAKE.

BODI YA WADHAMINI NA WAFANYAKAZI WA ZSSF WANAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA WA 2018 NA UWE WENYE MAFANIKIO

LIMETOLEWA NA:
 MKURUGENZI MWENDESHAJI
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR,
S.LP 2716 KILIMANI MNARA WA MBAO 


No comments:

Post a Comment