MAKAMU wa Rais Mstaaf Dkt
Mohammed Gharibi Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati akiwasili katika viwanja vya
maisara kuhuhudhuria sherehe za Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW,
yaliofanyika Kitaifa katika viwanja vya maisara Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimia na
Mwenyekiti wa Kamati ya Maulid ya Mfungo Sita Zanzibar Sheikh Shirali
Champsi alipowasili katika viwanja vya maisara Zanzibar kuhudhuria
katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimiana na
Makamu wa Rais Mstaaf Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipowasili katika
viwanja vya maisara kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
yaliofanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Al Hajj Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi
mbalimbali wa Dini na Serikali wakiwa wamesimama wakati wakutoa Salamu
za kumkaribisha qaswida iliokuwa ikisomwa na Madrasatul E Itiswam ya
Chukwani Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein akiwa na Wananchi na Viongozi wakisimama wakati wa
kutoa salamu ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Alhajj Ali Mohamed Shein alipowasili
katika viwanja hivyo kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad
(S.A.W)
WANAFUNZI wa Madrasatul E’itiswam
ya Chukwani Zanzibar wakisoma Qwasid ya Salamu ya kumkaribisha Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al Hajj, Ali Mohamed
Shein, katika viwanja vya maisra Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt Alhajj Ali Mohamed Shein, alkisoma ratiba ya
hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika
viwanja vya maisara kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar
Kabi na kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
KADHI Mkuu wa Zanibar Sheikh
Khamis Haji akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa hafla ya Maulid ya
kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara
Zanzibar
BAADHI ya waalikwa katika hafla ya
Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakifuatilia hafla hiyo
katika viwanja vya maisara Zanzibar
Picha na Ikulu
No comments:
Post a Comment