Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa mud wa siku 30 kwa
wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar
e s Salaam (TPA) ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza
haraka kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya
kuyatelekeza bandarini hapo kwa muda wa miaka 10 sasa huku mengine
yakitelekezwa pasipo kuwa na vibali maalum.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangallaakitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.
Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo la bandari ya nchi
kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa
bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya mbao zilizokutwa
bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena katika eneo la Malawi Cargo
Zoezi la ukaguaji likiendelea
Baadhi ya magogo yaliyokutwa bandarini hapo
Dk.Kigwangalla ametoa kauli hiyo
baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo kukagua mali na bidhaa
zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo katika zkukagua kwake huko
alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo yapo kwa miaka 10 sasa
ya...
kihifadhiwa huku wahusika wakishindwa kujitokeza.
“Naagiza mamlaka zilizo chini ya
wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote yalipo hapa bandarini.
Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya magogo 938, Ndani ya siku 30
mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze vinginevyo itabaki kuwa mali
ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.
Hata hivyo aliagiza pia kontena
55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo pia nazo wahusika wajitokeze
na nyaraka zao kamili ili waeleze kama kweli wameyatoa Zambia magogo
hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na wasipofanya hivyo ndani ya siku
hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Katika ziara hiyo, Waziri
Dk.Kigwangalla aliweza kutembelea bandari ya Dar es Salaam pamoja na
maeneo yanayohifadhiwa magogo hayo zikiwemo bandatri ya nchi kavu ya
NASACO, Malawi (Malawi Cargo) na baadae eneo hilo la bandari ya Dar es
Salaam.
Akiwa katika eneo la Malawi
Cargo, Waziri Dk. Kigwangalla aliweza kushuhudia makontena mbalimbali
yakiwemo yale ya mbao aina ya mitiki ambayo inatarajiwa kusafirishwa
nje ya nchi huku akibaini uwepo mkubwa wa udanganyifu kwa wasimamizi wa
upakuaji na usafirishaji katika eneo hilo la bandari ambao awali
walitaja idadi ndogo ya makontena ya mbao mbele ya Waziri hali
iliyopelekea kuanza kuyakagua makontena yote ndani ya eneo hilo.
No comments:
Post a Comment