Pages

Thursday, November 30, 2017

Wateja wa Tigo Kushinda Mamilioni ya Fedha Katika Promosheni ya Msimu wa Sikukuu


Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa promosheni ya ‘Fanya Muamala na Ushinde na Tigo Pesa’ jijini Dar es salaam leo, ambapo wateja wa Tigo pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi 15 milioni kwa kufanya miamala na Tigo Pesa. Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum, Mary Rutta na kulia ni Mkuu wa Huduma ya Tigo Pesa, James Sumari. 
Donge nono kushindaniwa kwa miamala yote ya Tigo Pesa
Dar es Salaam, 30 Novemba, 2017- Huduma ya fedha ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Tigo Pesa leo imetangaza zawadi kemkem kwa wateja wake ambao watajishindia mamilioni ya pesa kupitia promosheni ya ‘Fanya muamala na ushinde na Tigo Pesa’ inayoendeshwa katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya .

Promosheni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja itashuhudia washindi watatu wa jumla wakijinyakulia vitita vya TZS 15 millioni, TZS 10 millioni na TZS 5 millioni kila mmoja. Pamoja na hayo, kutakuwa na washindi wa kila siku ambapo mmoja atalamba donge nono la TZS 1millioni, huku wengine wanne wakijinyakulia TZS 500,000 kila mmoja, kila siku.

‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii,’ Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema akizindua promosheni hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Wateja watapata nafasi ya kushinda kwa kufanya miamala yoyote kutoka kwa simu zao kupitia Tigo Pesa. ‘Kadri ya unavyofanya miamala mingi zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda ,’ Sayed alifafanua. Hakuna masharti.

“Tunajivunia mchango wetu katika kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha nchini kupitia Tigo Pesa. Tigo Pesa ni zaidi ya huduma ya kutuma na kupokea pesa. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo tuna furaha kubwa kuwapa fursa ya kujishindia zawadi hizi nono ambazo zitawawezesha kufurahia msimu hu wa sikukuu huku wakiendelea kufaidika na huduma zetu bora za kidigitali,’ aliongeza.

Zawadi hizi murwa zinakuja kwa nguvu ya mtandao mpana na ulioboreshwa wa Tigo, huku lengo kuu la Tigo likiwa ni kuwasikiliza wateja wake na kuwapa huduma za kisasa zinazoendana na mahitaji yao.

Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini yenye mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 70,000 waliosambaa kote nchini. Miamala ya takriban TZS 1.7bn inafanyika kupitia Tigo Pesa kila mwezi.

No comments:

Post a Comment