Pages
▼
Tuesday, October 31, 2017
WANAFUNZI 448 WANAFUNDISHWA NA WALIMU 6 KATIKA SHULE YA MSINGI MDEKE ILIYOPO WILAYA YA KILOLO
Afisa mtendaji wa kata ya Ng’ang’ange bwana Aron Mwenzegule akiwa mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela wakibadilisha mawazo wakati wa ziara ya kutembelea shule ya msingi Mdeke
Mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce akizungumza mbele ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakati wa ziara ya kubaini changamoto za shule hiyo
Mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela akiwa makini kusikiliza anachoambiwa na mwalimu wa shule ya msingi Mdeke wakati wa ziara yake katika shule hiyo.
Na Fredy Mgunda,Kilolo.
Shule ya msingi ya Mdeke iliyopo kata ya Ng’ang’ange wilayani kilolo ina walimu 6 wanaowafundisha zaidi ya wanafunzi 440 na kusababisha kutotolewa kwa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Hayo yamebaini wakati wa ziara iliyofanywa na wajumbe wa kati za siasa wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani kilolo walipokuwa wameenda kwa lengo la kufanya usafi katika kata ya Ng’ang’ange
Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce alisema kuwa shule inajumla ya walimu 9 lakini walimu walimu watatu wameenda kusoma hivyo walimu waliopo shuleni ni walimu sita na kusababisha ugumu wa kuwafundisha
No comments:
Post a Comment