Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina (kulia) akiongea na team ya Wilaya ya Kasulu iliyoshiriki katika
zoezi la kukamata ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda, waliovamia
katika kijiji cha Kakere, kushoto kwake ni kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Bi.
Mwanahawa Mrindoko.
Katika Picha Ng’ombe aina ya
nyankole kutoka Rwanda, waliotaifishwa na serikali katika kijiji cha
Kakere wilayani Kasulu wakisubiri kukamilika kwa taratibu za mahakama
kwa ajili ya kupigwa mnada.
Waziri Mpina akiongea na
wanahabari hawapo katika picha baada ya zoezi la kutaifisha kundi la
ng’ombe waliovamia katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina, akiangalia Ng’ombe aina ya nyankole waliopo katika kijiji cha
Kakere baada ya kutaifishwa na serikali.
………………
NA; MWANDISHI MAALUM – KASULU
Kufuatia zoezi linaloendelea la
oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine
imetaifisha kiasi cha ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere
wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Akiongea katika zoezi hilo Waziri
Mpina amesema Wilaya za mipakani mwa Nchi jirani ziko katika tishio
kubwa la kuvamiwa na mifugo na kuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu
kuanza kuandaa utaratibu wa ...
mahakama kuzipiga mnada. “Hatua ya kwanza
sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa
kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo
ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama
No. 17 ya mwaka 2003.” alisema Mpina.
Mpina aliongeza kusema kuwa,
ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu
zitakapo kamilika, na kuitaka kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Kasulu kuelendelea kwa kasi kubwa kukamata mifugo katika mapori na
kuhakikisha mifugo yote inapatikana.
Sambamba na hilo, Waziri Mpina
aliwataka wananchi kujiadhari na kuondoka katika kununua kesi
zisizokuwa za kwao kwa kuikubali mifugo kutoka nje ya nchi kuwa ni ya
kwao, kwani ni kujitaftia matatizo na kuisadia serikali katika jitahada
hizi za kukamata mifugo inayoingia ndani ya nchi kinyume na taratibu.
“Kwa hiyo wananchi wawe namba
moja kuwafichua watu hao, na wale tunaowabaini kuwa wanaitikia mifugo
toka nje ya nchi kuwa ni mali yao lazima wachukuliwe hatua.” alisisitiza
Mpina.
Awali akitoa taarifa ya ng’ombe
hao waliokamatwa katika Wilaya hiyo mkuu wa wilaya hiyo Mwanahawa
Mrindoko alisema ng’ombe hao ni mali ya raia wa Rwanda kwani Serikali
ya wilaya ilikuwa inawatafuta Raia wahamiaji haramu na kuwapata, hivyo
sheria itachukua mkondo wake, na aliongeza kwa kusema kuwa kamati ya
ulinzi na usalama itaendelea na zoezi la kuwatafuta wafugaji ambao ni
wahamiaji haramu.
Akiwa katika wilaya ya Kakonko
Waziri Mpina aliagiza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo
kupitia Mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagalla kuanza mara moja zoezi la
oparesheni ya kukamata mifugo toka nje ya nchi kwani tarifa za awali
zinasema kuwa Wilaya hiyo ilikuwa haijaanza kabisa kutekeleza agizo hilo
na ni moja ya Wilaya ya mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.
No comments:
Post a Comment