Waziri
wa ujenzi,uchukuzi na mawasilino, Profesa Makame Mbarawa mwenye kofia ya njano
akiwa katika majukumu ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza
inayojengwa mkoani Pwani.
Mkurugenzi
mkuu wa mamlaka ya bandari Tanzania (TPA) Eng. Deusdedit Kakoko akifafanua
jambo kwa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasilino, Profesa Makame Mbarawa
alipokagua maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu ya Kwala –Vigwaza mkoani Pwani.
NA
WUUM, PWANI
WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea
kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala
Vigwaza Mkoani Pwani na kumtaka mkandarasi Suma JKT kuongeza kasi na kuzingatia
ubora.
Akizungumza
mara baada ya kukagua ujenzi huo ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA),
kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS) kuhakikisha wanaunganisha kwa haraka ili reli na barabara zinazoingia
katika bandari kavu hiyo zinakamilika na hivyo kuiwezesha bandari kavu hiyo kuanza
kutumika ifikapo Januari mwakani.
“TPA,
TRL na TANROADS uzuri wote mko kwenye wizara moja shirikianeni na hakikisheni
kilomita 15 za barabara inayoingia kwenye bandari kavu hii na kilomita moja ya
reli zinajengwa haraka,” Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kuhakikisha
ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza unazingatia ubora na viwango vilivyopo
katika mkataba ili kuiwezesha kuhudumia zaidi ya makontena milioni moja kwa
mwaka na hivyo kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
“Hakikisheni
eneo la bandari kavu linakuwa na maegesho ya kutosha, taa, maji ya uhakika,
gari la zimamoto, uzio na mashine ya ukaguzi wa mizigo scanner itakayowezesha kupima kila mzigo unaopandishwa na kushushwa
katika eneo hili,” amesisitiza Profesa Mbarawa.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Kakoko amesema TPA imejipanga kuhakikisha ujenzi
huo unatumia gharama nafuu na mifumo yote ya teknolojia ya habari na
mawasiliano TEHAMA inakuwepo katika bandari hiyo ili kuiwezesaha kufanya kazi
kisasa na kwa ufanisi zaidi.
“Tukifanikiwa
kuhamia hapa mzigo uliokuwa unasafirishwa kwa siku saba sasa utatumia siku tatu
kufika Mwanza hali itakayovutia wasafirishaji wengi kutumia bandari ya Dar es
Salaam na hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuibua fursa za ajira,” amesema Eng.
Kakoko.
Bandari
Kavu ya Kwala –Vigwaza inayojengwa na Mkandarasi SUMA JKT ambapo takribani
kiasi cha shilingi bilioni 9 kinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ili kuboresha
huduma za usafirishaji katika bandari ya Dar es Saalaam ambapo zaidi ya hekta
500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambapo kwa kuanza hekta 120 sawa asilimia
24 zinajengwa katika awamu ya kwanza.
Waziri
wa ujenzi,uchukuzi na mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa
maelekezo kwa Eng. Charles Salu Ogare anayesimamia ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment