Pages

Tuesday, August 1, 2017

VIKOSI VYA MAJESHI YA SADC KUFANYA ZOEZI LA PAMOJA MKOANI TANGA

Msimamizi wa Zoezi la pamoja kwa vikosi
maalumu vya Majeshi
ya SADC ambalo limepewa jina la  Matumbawe,Meja Generali Harison Msebu
katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama kushoto akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na kuanza zoezi hilo ambalo litaanza
Agosti 2 hadi Septemba 1 Jijini Tanga,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella
VIKOSI vya Majeshi ya Nchi za
Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwaafrika (SADC SPECIAL FORECES) vimeamua
kupambana na ugaidi,Uharamia kwa kushirikiana kufanya zoezi la pamoja
lililopewa jina la “EX MATUMBAWE” ikiwa ni mkakati wa kutokomeza vitendo
hivyo.


Zoezi hilo litakaloshirikisha vikosi vya Makomandoo, Ndege za
kivita,meli za kivita na makomandoo watakao ruka na miavuli huku wote
kwa pamoja kutoka nchi zote shiriki watafanya mazoezi hayo kubadilishana
uzoefu litafanyika kuanzia Agosti 2 mpaka Septemba 1 mwaka huu katika
maeneo ya Mapango ya Mleni.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga,Msimamizi wa Mazoezi
hayo,Meja Generali Harison Msebu alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni
kufanya mazoezi ya pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi ya SADC,ili
kuviwezesha kuwa na utayari na harakati katika kupambana na matishio
mbalimbali ya usalama.


Aidha alisema kuwa kutasaidia kuviwezesha vikosi hivyo kukabiliana na
masuala ya Ugaidi,Uharamia na maafa yatokanayo na  mabadiliko ya hali ya
hewa na kusaidia vikundi vya kulinda amani kama ilivyoelekezwa na
Jumuiya ya SADC pamoja na umoja wa Afrika (AU).


Alisema Nchi za Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Mwaafrika zimejiwekea
mikakati ya kuondoa uhasama wao na zaidi kuunganisha mahusiano ikiwa na
lengo la kupambana mambo ambayo yanaweza kuleta madhara katika nchi zote
za Jumuiya hiyo na Afrika kwa ujumla.
Alisema yapo madhumuni ya
kimkakati,utendaji kivita na kimbinu haya yote yakitekelezwa kwa ufanisi
zaidi kwa nchi zote upo uwezekano wa hali ya juu katika mafanikio ya
mapambano ya kigaidi na kiharamia.


“Tunajenga misingi mizuri kwa majeshi yetu na kuondoa dhana ya kupambana
wenyewe kwa wenyewe sasa tunaelekeza nguvu zetu katika mapamabano ya
kigaidi na kiharamia zaidi jambo ambalo litasumbu katika nchi hizi za
Afrika”Alisema Meja Jenerali Masebu.


Alisema zoezi hilo litashirikisha Nchi saba za Jumuiya hiyo zikiwa
Botswana,Lesotho,Malawi,

Jumuiya ya Afrika ya kusini,Zambia, Zimbabwe na
Tanzania ambao ndio watakauwa wenyeji
katika zoezi hilo ambalo

linafanyika hapa kwa mara ya kwanza.

Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigela aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi
pindi watakapokutana na vikosi hivyo vikiwa vinaendelea na majukumu yao
huku akiwataka kutoa ushirikiano pindi watakapo hitajika.


Alisema wananchi wasiokote vitu vyovyote wasivyovielewa na watoe taarifa
katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kitu ambacho watakiona kinawapa
mashaka.
 Habari kwa Hisani ya Blog
ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment