Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Serikali kupitia ofisi ya Madini
Kanda ya Kati imetakiwa kutoa elimu ya uchimbaji madini kwa wachimbaji
wadogo wa madini ilikuondoa migongano na migogoro ambayo imekuwa
ikitokea mara kwa mara pindi wachimbaji wanapovumbua maeneo ya madini na
kujikuta...
maeneo hayo wanapewa wachimbaji wakubwa bila kujali wachimbaji
waliokuwepo awali.
Kauli hiyo imetolea kwa nyakati
tofauti na wachimbaji wa Dhahabu kwenye Kata ya Changaa Wilayani Kondoa
walipokuwa wakijadili zuio la uchimbaji wa eneo walilokuwa wanachimba
tokea mwaka 2012 hadi suluhisho la mgogoro wao utakapopatiwa ufumbuzi
kwenye ofisi za Afisa madini mkazi Dodoma na kuzitaka mamlaka kuacha
kuwakumbatia wawekezaji na kuona wao ndio msingi kuliko wachimbaji
wadogo waliokuwa kwenye maeneo hayo kwa mda mrefu.
Wamesema kuwa Kabla mgogoro huo
haujaanza walikuwa wakichimba eneo la namba mbili na mwekezaji huyo
alikuja na kuwaondoa ambapo walisogea eneo la namba mmoja na kwa sasa
amekuja tena na kutaka kuwaondoa akidai kuwa amepewa leseni na kamishna
msaidizi wa madini na kuwa eneo hilo linamilikiwa na Kampuni ya Kondoa
Minning (T)Ltd.
Said Ramadhani ni mmojawapo wa
wachimbaji katika eneo hilo anasema kuwa kumekuwepo na sintofahamu ya
hatima ya wao kuendelea na uchimbaji baada ya barua ya Kaimu Afisa
madini mkazi Affa .E. Affa kuwataka kusimama kwa leseni za uchimbaji na
shughuli katika eneo la kijiji cha Changaa licha la suala hilo kuwepo
mezani mwao na majibu kutojibiwa kwa mda wa miezi miwili toka tar.24
mwezi wa 5 mwaka huu juu ya nani hasa ni mmiliki wa eneo hilo
linalogombewa kuanzia no 1 hadi 4.
Ramadhani alisema kuwa licha ya
kutuma maombi ya leseni ya umiliki wa eneo hilo wanaona wachimbaji
hawatendewi haki wakiambia Kondoa minning ina leseni na wao wakiambia
leseni zao zimefutwa hali inayowachanganya hadi sasa kuhusiana na sakata
hilo na kuiomba serikali kuja kutoa elimu kwao kuhusiana na suala zima
la madini ili waweze kuwalipa mrabaha na kodi ya serikali kwani hawana
wasi wasi na ulipaji.
Nae Mwenyekiti wa Kikundi cha
Kumucha Donmillan Shirima alisema wanaheshimu maamuzi ya Afisa Madini
Mkazi Dodoma na watayazingatia ila muda wa majibu yao umechukuwa mda
mrefu ikizingatiwa wao wanategemea suala la uchimbaji kuendesha maisha
yao ya kila siku kwani miezi miwili ni mingi nab ado majibu hayajatoka
tokea zuio lilipotangazwa Tar.24 ya mwezi 5 mwaka huu.
Shirima alisema kuwa wao wamekuwa
wakitii agizo hilo ila mwekezaji huyo ambaye anashirikiana na wabia
kutoka nchini Kenya kwenye umiliki wa hisa za kampuni hiyo bila kufuata
sheria za madini na ofisi ya madini kubariki kuwapa leseni na kuaacha
maombi ya awali ya kikundi hili linatuweka kwenye njia panda kujua hatma
yetu kwani suala hapa ni uvunjaji wa sheria za madini uliofanywa na
Kampuni hiyo ya Kondoa Minning iliyochini ya mwavuli wa Kampuni ya Kidee
Minning (T)Ltd
Wakati huo huo Kamishna wa Madini
Kanda ya Kati alipotakiwa Kutoa Majibu ya Wachimbaji Hao aliliambia
Gazeti hili kuwa kwa kuuliza hao wachimbaji wana chimba kisheria kwa
kufuata kanuni za baruti na wanananunua wapi, ila suala hilo lipo
mikononi mwa Ofisi ya Madini ya mkazi Dodoma na yeyeto anaetaka majibu
awasiliane nao ilikujua majibu ya nini kinaendelea kwenye kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo.
Alipotafutwa meneja wa kampuni ya
Kidee Minning ambao ndio washirika wa Kondoa Minning Ismail Kidee
alisema kuwa suala hilo wao wana leseni na kweli waliwakuta wachimbaji
hao kwenye eneo hilo na kuahidi kushirikiana na wachimbaji hao katika
kuhakikisha wanapata haki yao kama alivyoaahidi kwenye mkutano mkuu wa
Kijiji cha Changaa mwaka 2015.
Sakata la hatua ya ofisi ya Afisa
madini mkazi kutoa Zuio la leseni za Uchimbaji wa Madini kwenye Kijiji
cha Changaa na kuundika barua bila kuwepo muhuri limewaacha wachimbaji
njia panda na kuitaka kuhakikisha suala lao linapitiwa bila kuangalia
nani nacho na kuzitaka mamlaka kuwa makini na kusogea kulitazama suala
hilo kwa ukaribu.
Mogogoro wa eneo hilo unaogombewa
na Kikundi cha Kumucha ambapo wachimbaji wadogo ndio wanachama wa
kikundi hicho pamoja na Kampuni ya Kidee yenye Ubia na Kondoa Minning
huku wengine wakiwa ni Kampuni ya Millenium Builders Ltd ambapo mvutano
huo umekuwepo tangia Tar.8 mwezi wa Tatu mwaka huu baada ya uongozi wa
Kijiji cha Changaa na Mtaa wa Tumbelo kuitambulisha Kondoa Minning kuwa
inamiliki eneo hilo na kuwaacha wachimbaji wadogo kutojua hatma yao
licha ya kuvumbua madini hayo na kutuma maombi ya kuomba leseni
kutotimia.
No comments:
Post a Comment